Inatakiwa aanze hatua za mwanzo kabisa kabla hajaenda mahakamani.kama ni mkristo inampasa apitie kanisani walipofunga ndoa,aeleze hali ilivyo.Hapa inatakiwa kuwe na sababu maalum ya kuvunja ndoa hio. Hapa kama mume ndio aliemuacha mke, basi mke anaweza kutumia sababu ya kutekelezwa( desertion, abandonment). Kanisa wakishindwa kusuluhisha watatoa cheti,barua inayoonesha wameshindwa kusuluhisha,na hatua za mahakamani zitafuata.Cha kuzingatia inatakiwa kuwe na sababu kubwa ambayo haifai kurekebishika na ndoa imeharibika kabisa 'irrepeably broken' ndio talaka kuweza kutolewa.Habari za asubuhi wana Jamii forum wenzangu.nahitaji msaada wenu maana kuna mambo nahitaji kuyaweka sawa kwa jirani yangu .
JIRANI AMEACHANA NA MUME WAKE LAKINI MUME HATAKI KUTOA TALAKA,YAPATA MWAKA NA NUSU SASA.HIVYO ANAOMBA KUJUA KAMA ATAWEZA KUPATA TALAKA KWA AMRI YA MAHAKAMA ILI TUU AOLEWE NA MTU MWINGINE MAANA AMESHAMPATA.SASA AFUATE TARATIBU ZIPI ILI AWEZE KUPATA TALAKA YAKE KWA KUPITIA MSAADA WA SHERIA??