Sasa iko hivi, kwanza huajasema mkataba wako wa kazi unaisha lini, unaposaini mkataba wa ofisi ujue tu kwamba ofisi inaweza ika terminate mkataba wako muda wowote utakapo patikana una makosa ambayo utaratibu wa kuhojiwa umefuatwa na ukaonekana kuna makosa, inategemea wanaweza wakakusamehe au hapana, mara nyingi ofisi inaangalia security ya mali zao na fedha zao, Benki kuisainisha ofisi barua ili wakupe hela ilikuwa ni kujiridhisha kuwa wewe ni mfayakazi pale na mwajiri wako awahakikishie kuwa mkopo ule utaweza kulipwa kutokana na mshahara unao upata, mabenki mengi huwa yanawaomba waajiri kuwasaidia na taarifa pale ambapo kutakuwa na tatizo ili wasipoteze dedha zao, ofisi nyingi ukipatwa na kitu huwa wanakusimamisha kazi kwanza hadi hapo uchunguzi utakapo malizika ila wao huwa wanataswira ya kesi iliyopo kuwa either utapona au hutapona sasa wanacho kifanya ni kuzuia kwanza mshahara wako endapo una daiwa na ofisi hata mafao yako ili ikitokea umetoka salama watakulipa mishahara yako yote na mafao ambayo yalikuwa yamezuiliwa. ofisi kuzuia mshahara kwa sababu una makosa na umesimamishwa kazi na uchunguzi unaendelea inaweza ikawa sawa au isiwe sawa kwanini: kwasababu wao wanahisi unaweza ukaamua kukimbia kwakuwa una makosa na ukawa umeshapokea mishahara yako yote, kwa usalama zaidi wanazuia mishahara ili wajilipe madeni kwakuwa una matatizo kazini na wakuachie mshahara ambao utakuwa hudaiwi, boss wako kuongea na benki wakate deni ni kutokana na wao kuwahakikishia kuwa awali walikukabidhi kwao ukopeshwe ila kwa sasa hawako tena na wewe na hawataki kuulizwa badae.
Sasa iko hivi ukiona bossi ana Loby kuwa u resign usiendelee na kazi ni kosa kubwa sana maana yake wanaona iyo kesi utaishinda na ukishinda unaweza ukaishitaki ofisi kwa kuku chafua hata hivyo ukiwa nje bado tu unaweza ukawashtaki so hawataki uinshinde ukiwa upo kazini kwa sababu kuna mambo ya hapo kazini walikuwa wamesha ku exclude hawataki uendelee.
Ushari 1.Acha wafanye wanayo yafanya kesi ikiisha maana utakuwa na ushahidi wa kesi kuisha na hukuwa na hatia ndio uanze kufuatilia mafao yako ambayo utakuwa uliyapoteza ili urudishiwe 2. kama mkataba utaisha kabla ya kesi kumalizika na mishahra yako yote hukuipata basi watakulipa yote kwa wewe kuandika barua ya kuomba ulipwe mishahara yote maana bado ulikuwa ni mtumishi, japokuwa kuna terms za kwenye mkataba ambazo zinaweza zikasema kuwa mtu akiwa na matatizo na ofisi atasimamishwa na atavumiliwa kwa kipindi flan na baada ya hapo ataachishwa kazi kwa lazima, hilo ni la kuangalia. 3. Boss wako alitakiwa aendelee na mkataba wa kukata pesa zako kwa utaratibu ambao mlio jiwekea maana bado ni mfanyakazi sio lazima akate wote kulazimishwa mu resign ilikuwa ni njia ya kukutoa kwenye reli na pesa za ofisi azipate zote kwa pamoja. kwasasa usimshitaki bosi wako maana hutashinda kwa sababu bado kama mkataba wako uko hai na kesi haijaisha lazima atakushinda hapa ni kwenda taratibu sana umalizie kesi Loby na wewe kesi iishe haraka ili uanze kudai haki zako, mfano kama uliahidiwa baada ya kipindi flan unatakiwa upate kitu flan na hujapata kwakuwa ulisimamishwa kazi...
USIMSHTAKI BOSS WAKO KWANZA ACHA, medeni ya benki na kwa mwajiri wako acha wachukue ni pesa zao wanahaki ya kuzihitaji muda wowote wanapoona kua inafaa kutokana na misukosuko ambayo wanaona inaweza ikasababisha hasara kwao. subiri kesi iishe.