Msaada wa Kisheria

Sina barua ya mimi kutoenda kazini,nilimuuliza boss akasema ongea na wakiliwa pia akatuma namba, wakili ndiye wa kwanza kusema mimi ni design nikakataa
 
1. Ni kosa kubwa sana wewe kutokwenda kazini hii inaweza ikawa basis ya kukuachisha kazi kama mkataba unavyosema kuwa usipoonekana kazini ndani ya siku kazaa mkataba wako utakuwa terminated iyo ni moja ya kosa inayoweza kufuta mkataba wako, 2. unatakiwa kuwepo kazini mpaka hapo utakapokuwa umepewa barua ya kusimamishwa au notisi ya kusimamishwa kazi, unaweza ukaenda ukafikia ofisini kwako kama kuna kazi unafanya kama hamna unakaa tu mpaka bosi wako akupe barua ambayo itakuwa ina sababu za wewe kusimamishwa. 3. Hata sasa hivi wakikataa kukulipa mshahara wana haki kwakuwa hauonekani kazini. 4. Kazini kuna register mnapo ripoti kila siku hii inaonyesha rekodi ya mahudhurio yako kazini hii ni muhimu sana signature yako kuonekana umeripoti huko. 5. J3 nenda kazini moja kwa moja uonane na Boss wako ana kwa ana umeueleze unarudi kazini kwakuwa huoni kinachokufanya ubaki nyumbani na usiendelee kufanya kazi umsikilize atakavyo kujibu maana hata mwanasheria hana haki ya kukushawishi uache kufanya kazi eti u resign sababu ni ipi hana sababu yoyote. kama polisi wameshatoa ripoti na umekuwa mtuhumiwa akueleze ujue na ofisi ikupe kwa maandishi. Umenielewa hapo, una swali
Hapana mkuu kazini siendi
.
 
Iko hivi naona hata ww hujaelewa, ukiambiwa mtu ana mkataba wa kudumu maana yake mpaka afikie umri wa kustaafu yan miaka 55 au 60 ndio mkataba wake utakuwa umeishia hapo. umeelewa sasa
Kampuni ikifa?
 
Mkuu nimekuelewa, je kwa hapa nilipofika naweza kwenda ofisini au niulize kuwa kama naweza kwend kwa bosi? Mana nilipopata dhamana niliuliza kuwa niende bosi akasema, niongee na mwanasheria wake,
 
Mwanasheria huwa ni wa ofisi sio wa mtu binanfsi na kama ofisi au kampuni haina mwanasheria badala yake anamtumia wakwake binafsi kama consultant kwa kampuni basi, laikini iwe siri yako ni kwamba waki review mkataba wako unavyosema basi wanaweza waka terminate. sasa nakushauri hivi ila tatizo sijui kosa lililowafanya mpelekwe polisi nijue kama ni kosa ambalo linaweza likafikirika kurudishwa kazini au la. (njoo PM unambie kosa ili nipate wazo lingine na kipi cha kufanya) ujue unapoomba kutaka msaada wa kisheria ukiwa msiri huwezi saidika tunaweza tunazungumzia kitu kumbe yapo mengine nyuma ya pazia. sasa kabla sijaendelea pm kosa then nitaendelea
Mkuu nimekuelewa, je kwa hapa nilipofika naweza kwenda ofisini au niulize kuwa kama naweza kwend kwa bosi? Mana nilipopata dhamana niliuliza kuwa niende bosi akasema, niongee na mwanasheria wake,
 
Nakuja pm
 
Wakuu je kuna ofisi ama taasisi inayoshughulikia maswala kama haya ama kutoa msaada?
 
Mkuu Mungi umeongea kwa hisia zaidi japo sijamaliza kusoma!
 
Japo hujasema umeshtakiwa kwa kosa gani na lina uhusiano gani na boss, na ni hatua gani zimeshachukuliwa mpaka sasa dhidi yako, ila haya bado ni ya msingi;
1. Wewe bado ni mwajiriwa na hutakiwi kunyanyaswa au kupunjwa maslahi/ mshahara wako kwa vyovyote vile bila makubaliano yanayotengua yale ya awali.
2. Huyo boss wako naona ana-malice au siyo mwelewa.
3. Kama hujapokea mshahara wako ni kosa chini ya Sheria ya Ajira na Mahusiani Kazini na unaweza kufungua mgogoro wa maslahi katika Tume ya Usuluhishi na Uamuzi(CMA) ndani ya siku 60 tangu tatazo la kunyimwa/kupunjwa mshahara lilipojitokeza.

All the best!
 
Asante sana mkuu, lakini bosi mshahara alipeleka wote ila bank ndiyo waliamua kukata pesa yao yote kama rejesho kutokana na taarifa walizozipata kutoka kwa bosi. Kosa lilitendwa na manager wangu ambaye ni mtu wa karibu sana na mimi, so uchunguzi unafanyika kubaini kama nami nilihusika ama lah. Je bado ninaweza kwenda kufungua kesi ilihali ni bank ndiyo wamekata pesa yote?
Asante
 
Halafu hueleweki vizuri, kuna sehemu umesema boss alikukata mara benki n.k....Unapochukua mkopo benki, lazima kuwe na makubaliano ya jinsi ya urejeshwaji wa mkopo, kuwa watakata kiasi flani kwa mwezi. Kwenda kinyume na makubaliano ni kosa! Na sijui ni benki ya aina gani!
 
Nilikiwa na mikopo miwili, mkubwa wa bank na baadae nikakopa kwa bosi, mwezi huo huo niliyochukua mkopo kwa bosi ndiyo matatizo yalitokea kupelekea bosi kukata pesa zake zote mara moja tofauti na makubaliano ya kukata kwa awamu tatu. Kiasi kilochobaki alipeleka bank kama kawaida na bank wakakata pesa yao hivyo mimi mwezi huo (August) sikupata chochote. Mwezi September bosi alipeleka mshahara wote kwani yeye alikuwa hanidai tena lakini bank ndiyo na wao wakazui pesa zote. Natumai nimeeleweka mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…