Msaada wa kisheria

Msaada wa kisheria

Bubu Msemaovyo

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2007
Posts
4,120
Reaction score
3,468
Nina ndugu yangu alikuwa na kesi alishitakiwa kwa wizi wa matunda toka shambani. Aliyemshtaki ni mvamizi katika shamba hilo. Huyu ndugu yangu alikuwa anachunga matunda yake. Mvamizi huyu wa shamba ambaye anadai shamba na matunda ni vyake alienda mahakamani. Kesi imeendeshwa na kumpa ushindi huyu ndugu yangu. Akaachiwa huru baada ya hakimu kusema "Ushahidi ni wakujichanganya sana".

Mshitaki akakata rufaa. Akidai hajaridhishwa na uamuzi wa Mahakama. Anasema Mahakama haikuzingatia evidence alizozitoa hivyo anaiomba Mahakama ya Wilaya ipitie upya mwenendo mzima wa kesi.

Swali langu:
Huyu ndugu yangu ambaye mahakama ilimuona hana hatia hii karatasi ya rufaa anatakiwa afanyiwe nini kisheria? Je, kuna jambo anatakiwa kujiandaa siku ya kufika mahakamani?

Swali limekuja baada ya Hakimu kumwambia ndugu yangu aandae majibu ya kumjibu aliyekata rufaa. Je, ni sahihi? Kama hana imani na Mahakama ya Mwanzo mshitakiwa ajibu nini katika rufaa hii?
 
Kwa ushauri wa haraka wakati mnasubiri majibu humu, nendeni kwenye ofisi yoyote ya Mwanasheria mtapata ushauri kwa kina kwani mntaongea mambo mengi sana,ambayo huwezi kuongea humu.
Usishangae huyo alokata rufaa akaja humu kukupa ushauri wa nini cha kujibu
 
Inabidi aandae majibu ya kujibu ile rufaa ya mrufaani ndani ya siku 21 apeleke mahakamani, cha msingi achukue nakala ya hukumu na ile rufaa ampelekee mwanasheria amuandalie majibu.
 
 
Back
Top Bottom