Msaada wa kisheria

Msaada wa kisheria

evonik

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2015
Posts
3,996
Reaction score
5,156
Habari zenu wakuu,

Niingie kwa mada, kuna ndugu yangu alikuwa na duka la vyakula la rejareja lakini mapema mwaka huu (2019) aliamua kulifunga kwa kufuata taratibu zilezile alizotumia kulifungua. Kwanza aliandika barua na kuiwasilisha TRA kuwa anataka kufunga biashara yake hiyo, barua ikapokelewa kisha akaamua kufanya kama alivokusudia (kufunga biashara)

Lakini imepita miezi sita, bado TRA wanamtumia SMS za kumkumbusha kuwa alipe kodi wakati alishatoa taarifa kuwa ameacha biashara hiyo, alienda TRA akaambiwa bado hajatolewa, hivyo karan mmoja akamwambia itabidi alipe hiyo kodi ya miezi sita ambayo alifunga biashara lakini akawa bado hajatolewa kwenye mfumo au kanzidata ya TRA, ndugu alichoka kusikia vile, bado anawaza atafanyaje na keshaambiwa alipe ili afutwe.

Mkasa huu naufananisha na ndugu yangu mmoja alikosewa jina kwenye kitambulisho cha NIDA tena yeye aliandika vizuri jina lake ila NIDA walivyoandika ni tofauti, akatakiwa kulipa Tsh 20,000/= ili arekebishiwe. Je, na vipi hili la TRA haliwezi kumcost kama la NIDA?

Msaada wenu wakuu, afanye nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom