Msaada wa Kisheria

Msaada wa Kisheria

Mtoto shamba kapewa na babake harafu akakuuzia wewe!, kuna uthibitisho wa umiliki wa mtoto kumilikishwa hilo shamba?, maana yaonekana kama mtoto kauza shamba lisilo lake.
HAPANA, KUNA MIRATHI YA BABU YAKE AKIMPA HILO ENEO. WALISHAGAWIWA MAENEO YAO NA KILA MOJA AKARIDHIKA. MSIMAIZI WA MIRATHI ALITOA USHAHID HUO NA WALIOTIA SAHIHI KWENYE WOSIA WOTE WALITOA USHAHIDI KUWA ENEO HILO NI LA MJUKUU ALIYENIUZIA.
nadhani huyu jmaa anakasirika mtoto ake kunuzia maana hawaelewani na baba yake .......
 
Asante.

Sikutaka kumpeleka huko kwenye kufungua kesi ya msingi (land application), zuio la muda (temporary injunction) na kuomba isikilizwe kwa haraka kwa kuweka hati ya dharura (certificate of urgency), kwasababu hizo ni hatua za mbele sana.

Yeye alitaka cha kufanya sasa kwasababu jamaa ameanza kuvuna miti.

Kwa sasa polisi wanaweza kumsaidia kwa kutumia nakala ya hukumu. Hapa itatumika busara na siyo Sheria, kwasababu so far, hata hao polisi hawamjui mmiliki halali.

Vinginevyo afanye kama nilivyoshauri mwishoni kwamba amuache aendelee kuvuna wakati huo afungue shauri la msingi, akishinda adai fidia.
Ushauri wako mzuri lakini kumwacha mtu akate miti, auze mbao Kisha wewe uje kufungua kesi baadaye kudai fidia Kwa system ya mahakama zetu, ni vigumu kupata haki. Mwenzako tayari atakuwa na Hela ya kuhonga polisi, hakimu, kuweka wakili wakati ndugu yetu hata mafuta ya kuwapa polisi Hana. Kuna baadhi ya polisi hawashughuliki na migogoro ya ardhi labda Hadi waone watu wanahatarisha amani au mauaji. Ni vizuri kuchukua hatua ya haraka afungue kesi Baraza na kuweka zuio.
 
Ndugu yangu, siku hizi hakuna kesi inayoenda Wilayani bila kupitia Kata isipokuwa kama imekaa Kata kwa zaidi ya mwezi bila muafaka kupatikana.

Na ukumbuke kwamba hakuna option ya ku-waive requirement ya kupita Kata kama ilivyo kwenye ile notisi ya siku 90 ukitaka kuishtaki Serikali.

Ni yaleyale tu. Mfumo wa Mabaraza yetu ya Kata unaujua? Sijakataa asiende moja kwa moja Kata na Wilayani, ila mazingira ya Kata tu siyo favourable.

Ndio maana nikasema the immediate and effective option ni kwenda Polisi kuomba busara yao akitumia Hukumu ya Mahakama. Nimeshafanya hii mara kadhaa na ika-work out.
 
Back
Top Bottom