Msaada wa kisheria

Msaada wa kisheria

jaqfantasy212

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2012
Posts
542
Reaction score
257
habari wanaJF..

Naomba ufafanuzi wa kisheria katika hili...

story ina mlolongo mrefu sana, ila naomba niandike kwa kifupi sana ili muweze kunielewa nahitaji nini hasa..

Baba alipofariki miaka 22 iliyopita aliacha vitu kama nyumba na mashamba kwa ajili ya mama na watoto, kila mmoja alikuwa amemuandikia apate nini, kwa kuwa alifariki tukiwa bado wadogo, vitu vyote alikuwa anaviangalia mama mpaka tulipokuwa wakubwa wa kujitegemea, mama aliamua kutuonyesha na kutupa kila mtu alichoachiwa japo hakutupa kimaandishi..

Tatizo ni hili, kwa upande wa kaka yangu yeye alioa akawa anaishi na mke wake kwenye nyumba aliyopewa, kwa bahati mbaya aliachana na mke wake takribani miaka saba iliyopita,mwanamke aliondoka na watoto..mwaka jana mwezi wa nane alifariki, shida ni kwamba mke wake amerudi na anataka mirathi ya marehemu mume wake..

swali langu ni je, ni haki yeye kupewa mirathi ya mumewe ingawa walikuwa wameachana?
pili ni lazima apewe yeye hata kama familia ya mume wake haina imani naye?
 
Mmmh nilisomaga zaman sana kimtindo kwamba mali za urithi wa mtu mmoja zilizopatikana kabla au baada ya ndoa hazimuhusu huyo so called mke..inabidi nikichekie ili niwe accurate na nachokisema na pia inategemea hiyo nyumba ni design ya joint property au personal property kwa maana kwamba hiyo nyumba imeandikishea jina la mtu mmoja au watu wawili mke na mume..pia..cheki tu na wasimamizi wa mirathi..kama vipi..kwani mnataka muichukue hiyo nyumba ama?
 
Back
Top Bottom