irumba1
JF-Expert Member
- May 10, 2013
- 882
- 321
Nilikuwa na mchumba wangu ambaye nilitaraji kufunga ndoa nae ya kiislam,maandaliz ya harusi yaliendelea vizur sana na nilifanikiwa kujitambulisha kwao na pia kulipia mahari kwa asilimia 85,lakin baada ya kulipia mahar wazazi wake wakawa wananilazimisha nifanye haraka hiyo harusi lakini kutokana na mimi kuwa mbali kikazi niliwaomba wanivumilie.hata hivyo baada ya miezi kama 6 toka nilipolipa mahari wale wazazi wakaruhusu binti yao akaolewa na mtu mwingine,Sasa wana jf haki yangu ni ipi katika hili?,nidai mke au nidai mahari?,sheria za kiislam zinasemaje? Na je sheria zetu kwa ujumla zinasemaje kuhusu hili?.msaada please