Msaada wa kisheria

Jomba Wajo

Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
33
Reaction score
17
Mimi ni mwajiriwa wa kampuni moja binafsi iliyopo hapa jijini Mwanza kwa miaka miwili sasa. Niliajiriwa kwa mkataba wa miaka mitatu. Mwaka wa kwanza tuliumaliza bila matatizo lakini ulipoanza mwaka huu wa 2013 kumekuwa na matatizo makubwa ya mishahara kwa watumishi japo hatupo wengi sana.

Ni miezi saba sasa tunafanya kazi bila malipo yoyote ya mwisho wa mwezi. Mkurugenzi anaishi Dar na amekuwa akija na ahadi za uongo na mbinu za kutugawa. Mimi nimechoka naomba kwa wataalamu wa sheria wanijulishe ni hatua gani ambazo naweza kuchukua ili haki zangu zipatikane maana nimefatilia pia huko NSSF nayo yalikuwa hayapelekwi.

Naomba mnisaidie wadau bado sijachukua hatua yoyote ndo maana nahitaji maoni yenu kwanza.
 

Kama hawapeleki makato NSSF bas hilo ni kosa wanaiibia serikali watashugulikiwa na TRA ila wewe ishu yako waweza peleka malalamiko CMA utapatiwa haki zako ndan ya mda mfupi na reliable unaweza pia kwenda labour court ila itachukua muda mrefu. Utaratibu wa jinsi gan ukafungue shauri CMA mtafute mwanasheria hapo Mwanza nenda ata Ofisi za msaada wa sheria km Nola au LHRC watakusaidia binafsi niko dar ningeweza kukusaidia km ningekua Mwanza.
 
Poleni, miezi 7 bila mshahara? Majanga!
 
Mkuu kama ni hivyo wahi kafungue shauri CMA. Kutokulipwa mshahara miezi 7 inapelekea 'constructive termination'/mwajili amefanya mazingira ya kazi yawe magumu na imekuwia wewe ugumu kuendelea na kazi. Ufungue kesi yako CMA maana kesi zote za kazi zinapaswa kuanzia huko. Pia unapaswa kujaza form No 1 pia kumbuka form inajazwa ndani ya siku 30 toka mgogoro utokee, ukiwa nje ya muda ujaze fomu No 7 inaitwa 'condonation form' kwa ajili ya kuomba kufungua kesi nje ya muda. (Usiandike barua ya kuacha kazi).
 
Hiyo kampuni ina-deal na nini? Kungekuwa na fixed assets, basi mngezitwaa na kuziuza kish mjilipe mishahara labda huyo employer wenu ndio angetia akili
 
assets zipo tena za thamani kubwa ninachohitaji ni kuchukua uamuzi ambao unalindwa na sheria. kama sheria inaruhusu kuuza mali za mwajiri na kujilipa its ok. lakini nahitaji niwe salama mbele ya sheria.
 
thanks mkuu. I appreciate your concern. je huko huwa haichukui muda mrefu sana?
 
Hiyo kampuni ina-deal na nini? Kungekuwa na fixed assets, basi mngezitwaa na kuziuza kish mjilipe mishahara labda huyo employer wenu ndio angetia akili


assets zipo tena za thamani kubwa ninachohitaji ni kuchukua uamuzi ambao unalindwa na sheria. kama sheria inaruhusu kuuza mali za mwajiri na kujilipa its ok. lakini nahitaji niwe salama mbele ya sheria.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…