Jomba Wajo
Member
- Apr 6, 2012
- 33
- 17
Mimi ni mwajiriwa wa kampuni moja binafsi iliyopo hapa jijini Mwanza kwa miaka miwili sasa. Niliajiriwa kwa mkataba wa miaka mitatu. Mwaka wa kwanza tuliumaliza bila matatizo lakini ulipoanza mwaka huu wa 2013 kumekuwa na matatizo makubwa ya mishahara kwa watumishi japo hatupo wengi sana.
Ni miezi saba sasa tunafanya kazi bila malipo yoyote ya mwisho wa mwezi. Mkurugenzi anaishi Dar na amekuwa akija na ahadi za uongo na mbinu za kutugawa. Mimi nimechoka naomba kwa wataalamu wa sheria wanijulishe ni hatua gani ambazo naweza kuchukua ili haki zangu zipatikane maana nimefatilia pia huko NSSF nayo yalikuwa hayapelekwi.
Naomba mnisaidie wadau bado sijachukua hatua yoyote ndo maana nahitaji maoni yenu kwanza.