the locksman
JF-Expert Member
- May 5, 2012
- 1,102
- 355
Poleni na majukumu wakuu! Naomba msaada wa kitabibu! Ni siku nyingi sasa nashindwa kula chakula vizuri nikashiba na kuridhika. Mara nyingi nakunywa chai asubuhi mlo wa mchana sipati maana nikila tu napata kichefuchefu na kupelekea kutapika, Makohozi huwa yanajaa kooni. Siku nyingine nakula milo yote bila shida. Najaribu kupima hospitali minyoo au taifod naambiwa sina, sijui labda vipimo si sahihi. Naomba anaye jua nifanyeje anisaidie.Ni miaka zaidi ya miwili sasa napata taabu.