Gily Gru
JF-Expert Member
- Jul 4, 2016
- 8,632
- 23,673
Wasalaam
Kuna jambo linamiumiza kichwa nimeshindwa hata kulala usiku huu nikaona niwashirikishe humu
Historia ya Charles David
Mtoto huyu ambae nimepata kufahamiana na mama yake kwa zaidi ya miaka 7 hivi. Kwa majina anaitwa Charles David. Hakuzaliwa na ulemavu, alipata ulemavu wa mwili na akili baada ya kuumwa degedege akiwa na miezi saba.
Baba yake mtoto ni teja teja wa madawa ya kuleva na mwizi mzoefu. Baba huyu hajawahi kuwa msaada kwa mtoto toka aingie kwenye madawa ya kulevya
Mtoto pichani soon anafikisha miaka 15👇
Kufahamiana na mama yake.
Nimefahamiana na mama mtoto tokea mwaka 2016. Anaitwa Maria.
Mtoto alipat kwend kituo cha walemavu masista Dodoma. Kipindi hiki uwezo wangu ulikuwa mzuri kifedha ada ilikuwa 130,000 kwa mwezi, ambapo nilikuwa namlipia mtoto ada ya kituo hapo Dodoma
Maria alikuja kuolewa na kupata mtoto wa pili wa kike.
Mwaka juzi baada ya kupitia changamoto mbalimbali za kifedha ikiweno mikopo bank nikashindwa kumgharamia mtoto. Hivyo kukawa na malimbikizo ya ada hapo kituoni
Mbali na mimi kumlipia mtoto Maria alishawahi kwenda clouds fm akapewa air time na kuweza kuomba msaada kwa watanzania, pia aliweza kupata msaada kupitia jumuiya, kanisa likamlipia kodi na gharama za hapa na pale za mtoto wake.
Baada ya kushindwa kulipa ada kwa miezi kazan, Kituo cha Dodoma kikatoa amri mama amchukue mtoto arudi nae nyumbani. Kwa maelekezo kuwa ameshindwa kulipa ada ya kituo na pili mtoto ana umri wa miaka 12 hivyo amevuka umri wa kuendelea kukaa kituoni
Mtoto alirudi nyumbani. Mme wake Maria amemtelekeza kwa sababu ya kurudi na mtoto mlemavu nyumbani na kumuacha na mtoto wake wa kike. Baba katelekeza familia japo alijua kuwa Maria ana mtoto mlemavu
Taratibu za kutafuta kituo kingine.
Maria anazunguka Kutafuta kituo ambacho kitampokea mtoto wake. Ila kila kituo anachoenda, anakataliwa kwa kigezo cha mtoto kuwa na umri mkubwa au kituo kimejaa
Ameshaenda vituo vingi sana vikiwemo kigogo, kigamboni, mtoni mtongani, mbagala zakiemu ..... na vituo vingi ambavyo sivikumbuki kichwani.
Wazazi wake Maria ni wazee. Baba yake ni mlemavu wa macho haoni. Angeweza hata kumuacha mtoto na mama yake ili yeye apambane kutafuta riziki, ila nyumbani kuna changamoto imemuwia vigumu Kuwaachia mtoto ili yeye apambane kutafuta.
She is the bread winner for the family, despite with heavy load, her responsibility is beyond her shoulders can bear. So sad...
Msaada Husika:
Msaada anaoomba Maria ni wa mtoto wake kupata kituo cha kulea watoto walemavu.
Akitoka asubuhi kwenda kufanya kazi ya mama ntilie, inamlazimu amuache Charles nje mwenyewe mpaka anaporudi saa tisa mchana.
Maoni Yangu
Mazingira anayoishi sio rafiki kabisa kwa mtoto wake. Hawezi kubaki nyumbani kwa sababu ni single mother na anapambana kupata kula ya watoto wake wawili.
Huyu dada anapitia changamoto kubwa sana hususani anafanya kazi siku tano katika juma. Japo weekend anapata mda mzuri wa kukaa na watoto nyumbani.
Kwa mazingira anayoishi mtoto si ya standard za haki za kibinadamu. Kuna mda mtoto anatambaa chumbani kwake na kumwaga ndoo za maji.
Mtoto anaingiza vidole kwenye cable za umeme. Chumba anachoishi ni cha elfu 30, chumbq kimoja. Anaishi na watoto wake wote wawili.
Kula ya hawa watoto ni shida, analipwa elfu 5 na boss wake kwenye kazi za mama ntilie. Siku nyingine hupewa chakula na boss kwa watoto ila sio siku zote.
Briefly:
Msaada wa kituo cha kulea watoto walemavu, mtoto ambae hajitambui kabisa.
Pia unaweza mwelekeza kituo akaenda kuomba msaada zaidi hapo. Jitihada za ustawi wa jamii kumpatia kituo umekuwa wa longolongo nyingi
Number za simu za Maria: 0716018180
Mungu awabariki sana. .