Msaada wa kuanzisha Kiwanda

Msaada wa kuanzisha Kiwanda

NAMTUMBA

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2014
Posts
1,939
Reaction score
597
Naomba msaada wa kitaalamu. Mm ni Mkulima wa Korosho huku Mtwara. Nimeuza shamba langu la Korosho kwa milioni moja na nusu (1,500,000) lengo langu ni kujenga kiwanda cha kubangua korosho ili kuunga mkono juhudi za awamu hii. Nimeona niuze shamba langu nipate mtaji wa kufungua kiwanda maana nimevutiwa sana na kasi hii. Nasikia nikiwa na laki tano naweza kuagiza kiwanda kizuri tu na chakisasa. Nisaidieni utaratibu namna ya kupata Kiwanda na jinsi ya kupata kiongozi mkubwa aje kuzindua na kukata utepe.
 
Mimi nakushauri kwanza fanya kitu kinachoitwa feasibility study ya project au mradi unao taka kuufanya kwa maneno mengine tembelea kwanza kiwanda chochote kile cha kubangua korosho uone mashine zake zilivyo na jinsi zinavyo fanya kazi na jaribu kutia mazungumzo na wa wahusika kuhusu upatikanaji wa mali ghafi na uendeshaji wa biashara kwa ujumla, kama uatabahatika, na kujua soko jinsi lilivyo ili upate idea jinsi gani utaendesha biashara au kusimamia mradi wako kikamilifu.

Wakati unafanya hiyo feasibility study angalia wapi wenzako wanafanya makosa na wewe ufanye nini ili uweze ku-compete. Usifanye kama wao fanya vingine kidogo kulingana na fantusy yako na utashi wako wa kuendesha kiwanda.

Usiende SIDO watakupiga porojo tu kwani wengi waliko huko ni wakatishaji wa tamaa. Nenda wizarani moja kwa moja ili wakupe mchango wao zaidi upate capital ya kutosha na za kukuwezesha wewe kupata mkopo wa kutosha bank ili uagize mitambo ya uhakika kwa ajili ya biashara yako.

Ukienda wizarani hakikisha kuwa una concept plan na business plan yako.
 
Naomba msaada wa kitaalamu. Mm ni Mkulima wa Korosho huku Mtwara. Nimeuza shamba langu la Korosho kwa milioni moja na nusu (1,500,000) lengo langu ni kujenga kiwanda cha kubangua korosho ili kuunga mkono juhudi za awamu hii. Nimeona niuze shamba langu nipate mtaji wa kufungua kiwanda maana nimevutiwa sana na kasi hii. Nasikia nikiwa na laki tano naweza kuagiza kiwanda kizuri tu na chakisasa. Nisaidieni utaratibu namna ya kupata Kiwanda na jinsi ya kupata kiongozi mkubwa aje kuzindua na kukata utepe.

Kwenye red hapo....

Pumbavu kweli.
Angalia Kama inakulipa Fanya ila sio kuunga mkono kujenga kiwanda lkn hakina faida.
wenye viwanda wanafunga Na ww unafungua kuunga mkono juhudi?

Hapa tunatafta Pesa hatuko kisiasa
 
laki 5 nyingi sana wewe nunua mawe tuu ya kuponda ponda na jiko la mkaaa la kuchomea / mfunguaji wa kukata utepe yupo tena anapenda kuuza sura tembelea karibu na feri muulizie atakuja anaitwa Juma pimbi masamaki/ ila lazima tukio liwe mubashara kma ni dark like bunge haji
 
Back
Top Bottom