salamu kwenu wanajamiii forum. Kuna jamaa yangu mmoja aliniuliza swali kuhusu kiwango cha uchukuaji mkopo kwenye taasisi za fedha akiwa na maana ya benki na hizi taasisi ndogo ndogo kama pride au finca au bayport. Swali lake lipo hivi kwa mfanyakazi kama yeye mwenye kupokea mshahara wa 390000 kwa mwezi anaweza kuchukua mkopo kiasi gani kiwango cha mwisho? Je anaweza kufikia milion 5? Malengo yake ni kuchukua ili afungue biashara zake ili kujikomboa na haya maisha ya mtanzania. Naombeni kuelimishwa kuhusu hili ili niweze kumshauri vema. Nawasilisha.
Mkuu,
kiwango cha kukopa kinategemea mambo kadhaa.
1. Mshahara wako, taasisi nyingine huzidisha mshahara wako mara namba fulani mfano 10,12,15 nk.
2. DSR - hii ni debt servicing ratio. yaani ni % ngapi ya mshahara wako italipia mkopo? hapa taasisi huweka kikomo/kiwango cha juu kabisa. wengine ni 33% hadi 50%
3. Riba - hii huathiri pia kiwango cha kukopa
4. Muda wa kulipia mkopo. hapa huanzia angalau miezi 12 hadi miezi 72.
kukusaidia inabidi kuweka "assumptions" kama ifuatavyo;
riba= 24%, muda wa kulipa = 60 months, DSR = 40% ya net yako, kwa mshahara wako na ikiwa utalipa makato sawa kila mwezi utapaweza kupata kama TZS 4,500,000 (tumechkulia hiyo 390,000 ni net pay yaani take home yako.
hata hivyo,
unapokopa kwa kutumia mshahara kuna mambo kadhaa ya kuangalia ikiwa ni pamoja na;
1. mwajiri wako anaweza kuhitajika kusaini makubaliano na taasisi zinazowakopesha. hii inasaidia kukusanya marejesho na ni rahisi kupata riba nafuu. shida ya hii ni kwamba unalazimika kutumia riba iliyokubaliwa hata kama taasisi nyingine sokoni zinatoa riba nafuu zaidi
2. mikopo ya aina hii hujulikana zaidi kama personal loans/consumer loans ambayo sana sana inatumika kufanya shughuli binafsi kama kununua samani, kulipa ada, kununua viwanja na wengine wanatumia kujenga. inapokuwa unataka kufanya biashara inabidi kufanya mahesabu ya ziada ya biashara yenyewe.
cha muhimu ni kwamba unapoamua kuchukua mkopo ni lazima ujipange na uhakikishe unaweza kumudu maisha ya kuulipa mkopo na kuhudumia familia kwa kilichobakia kama unayo. ni lazima upange kufanyia kitu kitakacholeta manufaa kwako.
siku hizi kuna credit bureaus, ukishindwa kulipa taarifa zako zinapelekwa huko kupitia benki kuu, madhara yake huko tunakoenda ni makubwa zaidi
Hao waote uliowataja hapo juu, riba zao ni 24% - 40% biashara ipi utatengeneza margin ya 26%? Zaidi ya biashara ya sembe au zekinana's
Mkuu! Kuna vigezo ambavyo financial institution huangalia,kama kiasi cha net salary yako,na dhamana unayotumia mara nyingi inakua ni michango yako ya mifuko ya jamii I.e Ppf,Nssf n.k,itakua ni upuuzi kwa benk kukupa mil 20,wakati Ppf yako ina laki 9,so kuna ratios ambazo huzingatiwa ili kutoa mkopo kulingana na mshahara wako pamoja na dhamana(social security fund contribution),na lazima ujue kwamba mshahara wako sio wako pekee,hata watoto ndugu wanautegemea ,so haiwezekani upewe mkopo ambao utasababisha kiasi kikubwa cha rejesho kuuservice mkopo,ndio maana mdau hapo juu alielezea concept ya DSR ambayo huwa calculated kwa kuchukua(Installment/payment capacity),huwa in % form,na maximum ya DSR hutofautiana bank na bank,niliyopo mimi max ni 80%,the minimum is better,Note:usichukue mkopo kwa muda mrefu sana maana kadri muda wa mkopo unavyokua mrefu ndio riba huwa kubwa this is principle hakuna ubishi juu ya hilo,then chukua ukiwa na malengo juu ya mkopo,usichukue kadri ya tamaa zako zinavyokusukuma.
Mkuu izo riba ni kwa mwaka au kwa mwezi!?,maana huenda watu hawaelewi somo la riba kwa kweli!,ukijibu tarudi tena
Well said mkuu,ndio maana kabla sijaanza kuchangia nilimuuliza mkuu watu,anielekeze hizo riba hapo juu alikua anamaanisha kwa mwezi au kwa mwaka,coz zilikua ni kubwa sana endapo ingekua ni kwa mwezi,but jibu lake akasema ni kwa mwezi kama ilivyo kwa rejesho,but kwa uelewa wangu hakuna benki inayoweza kuchaji kiasi cha 20%-40% kwa mwezi,maana huo ni ufisadi wa hali ya juu sana,nadhani mkuu hapo juu alikua anamaanisha kwa mwaka!Hili swala la riba ni muhimu kulielewa vizuri. Riba ina sehemu kuu tatu;
1. Kiasi cha riba yenyewe; hii ni ile rate, mf 20%
2. Namna invokokotolewa; hapa nimanisha frequency; mi kwa mwezi, mwaka, siku nk. Sasa elewa vizuri hapa. Taasisi nyingi hupenda kutaja riba ya mwaka ambayo inakokotolewa kwa mwezi. Mf riba ya 24% kwa mwaka ni sawa na 2% kwa mwezi.
Kuna taasisi fulani huwa wans riba ya 8%. Lakini ukifuatilia unakuta ni kwa mwezi. Maana yake ni kwamba hii ni 96% kwa mwaka
3. Riba inakokotolewa kwenye nini?
Hapa kuna namna nyingi lakini kuu ni deni lililobaki, kiwango cha hela ilichokopa bila kujali kama kinapungua au la.
Ushauri
Unavyokopa ni haki yako kupewa mtiririko wa jinsi utavyotakiwa kurejesha mkopo hadi mwisho na ni lazima huo mchanganuo uoneshe ni riba kiasi gani unakatwa.
Kama unaweza kutumia excel unaweza kujaribu hii kitu. Fungua new excel, peleka mouse palipoandikwa sheet1, right click, click insert.
Chagua other excel solutions, tafuta loan amortization schedule, click hiyo na itakuletea template ambayo waweza kutumia kupima kiwango cha mkopo
Mkuu izo riba ni kwa mwaka au kwa mwezi!?,maana huenda watu hawaelewi somo la riba kwa kweli!,ukijibu tarudi tena
Na hio mikopo ambayo ni unsecured inakua vipi kama una idea?Mkuu,