nundaz
JF-Expert Member
- Jun 8, 2012
- 272
- 193
salamu kwenu wanajamiii forum. Kuna jamaa yangu mmoja aliniuliza swali kuhusu kiwango cha uchukuaji mkopo kwenye taasisi za fedha akiwa na maana ya benki na hizi taasisi ndogo ndogo kama pride au finca au bayport. Swali lake lipo hivi kwa mfanyakazi kama yeye mwenye kupokea mshahara wa 390000 kwa mwezi anaweza kuchukua mkopo kiasi gani kiwango cha mwisho? Je anaweza kufikia milion 5? Malengo yake ni kuchukua ili afungue biashara zake ili kujikomboa na haya maisha ya mtanzania. Naombeni kuelimishwa kuhusu hili ili niweze kumshauri vema. Nawasilisha.