Msaada wa kuelimishwa MADAKTARI please!

Msaada wa kuelimishwa MADAKTARI please!

kiparah

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2010
Posts
1,173
Reaction score
117
Mimi, mtoto wangu mmoja wa kike na wadogo zangu wote wanne ni group 0+. Tatizo kubwa ni kuwa mafua ni tatizo kubwa mno kwetu, yaani yanatusumbua mno hadi mtu unalala, lakini magonjwa mengine kama malaria kwetu tunamshukuru Mungu hayatusumbui. Ningependa madktari mnisaidie kujua mambo haya:
Ina maana group hili kwenye virusi vya mafua liko WEAK SANA? au Virusi vya malaria viko WEAK SANA kwa group hili?
Naomba majibu yenu watalaamu,
Natanguliza shukrani zangu.
 
Ngoja watakuja nafikiri wanaandaa makala coz hili swali limeulizwa mara nyingi
Mimi pia ni mhanga na sijapata majibu bado.
 
kwa uelewa wangu mtu kupata magonjwa hakutegemei blood group. hayo mafua wewe na familia yako nahisi itakuwa allergy. allergy inaweza kurithiwa hivyo mnawezekana mnaallergy ya kitu fulani hasa kama mnaishi nyumba moja. cha msingi ni kujua ni kitu gani kinawasababishia allergy. mfano nilikuwa nakohoa kwa muda mrefu sana na mama yangu nae ilikuwa hivyohivyo. kumbe tatizo lilikuwa kwenye mablanketi tuliyokuwa tunatumia. baada ya kuacha mambo yakawa shwari. so angalia vitu ambavyo ni common kati yenu ambavyo vinaweza kuwa vinawasababishia allergy.
 
Back
Top Bottom