Pole sana mkuu, hilo tatizo lako nimelielewa vizuri sana kwasababu nilishawahi kupitia mtihani huo. Nilipokuwa chuo mwaka wa kwanza(Chuo nakihifadhi) nikiwa sina Girlfriend nikakamata msichana mmoja kwa ajiri ya kupotezea mda(kwa wakati ule nilimuona siyo mzuri sana ukilinganisha na wasichana wengine hivyo niliona huyu awe wa kupita tu) kadiri mda ulivyokuwa unakwenda ndipo akawa ananionyesha mapenzi ya hali ya juu sana ikafikia wakati hata upande wa kwetu yaani dada zangu, kaka zangu mpaka wazazi wakawa wanamfahamu, hii ni kutokana na ushiriki wake katika matatizo yaliyokuwa yanatokea nyumbani kwetu japo mimi kwao nilikuwa sitokei hata kama kuna msiba, nikiwa mwaka wa pili zoezi la kujitoa likaanza ili nitafute mtu nimpendaye. Nilimfanyia vituko vingi sana lakini haikuweza kutuachanisha na wakati mwingine nilimfanyia mambo ambayo yaliniumiza sana hata mimi kama binaadamu hatimaye mwaka wa Tatu nilifanikiwa kumpiga chini japo nilimsababishia matatizo makubwa mdada huyu mpaka akapata supplementary katika masomo mawili ambayo aliyarudia hakufanikiwa ku-clear somo moja, alirudia mwaka wa tatu mimi nikamaliza chuo nikaingia mtaani na nikapata kazi. Nikajikita na demu nimpendaye alikuwa pale IFM 2nd year (nilikuwa nimeanza ku-cheat naye wiki chache nyuma na ndiyo iliyonipelekea spidi kubwa ya kumpiga chini msichana niliyekuwa naye) nilispend naye for 8 months nikaachana naye kwa aliyonitendea(sitopenda kuyataja hapa kwani siyo jukwaa la wakubwa) Huwezi amini hapa ndipo nilipomkumbuka yule mdada niliyemuacha ningakundua mtu wa kuishi naye aangaliwe kwa factor zaidi ya moja. Binafsi yule msichana nilimuacha kwasababu tuu nilikuwa naona wasichana wengi wazuri zaidi yake, nilikaa kama miezi kadhaa sina permanent Girlfriend ndipo nikagundua hii siyo life maadamu niligundua makosa yangu nikafuatilia kama yule msichana ana mtu nikaambiwa hana mtu na amepoteza kabisa hali ya kuwa na boyfriend. Ilinichukua mda mrefu sana kumuelekeza kama najuta kwa niliyoyafanya nikamsisitiza kwamba nahitaji awe mama watoto wangu alinikatalia katakata hii ilikuwa mwaka 2005 mwanzoni, baadaye nikawatumia rafiki zake na nikawaambia ukweli kwa kila kitu mwishoni mwa 2006 nilikubaliwa ombi langu upya akiwa ndo amemaliza chuo, Harusi yetu ilikuwa mwanzoni mwa mwaka2008 na sasa tuna mtoto mmoja aliyepatikana mwanzoni mwa 2010, tunaishi vizuri tunaheshimiana na kutokana na tabia yake amekuwa ni mwanamke mzuri sana kwangu hanichoshi(NINAMPENDA SANA) japo najutia sana doa nililoliweka katika historia yetu. Plz nakushauri jiulize mara mbilimbili ni kitu gani kinachokufanya usimpende huyo mwanamke japo umekuwa naye for sometimes. Nimeiandika haraka lakini hii ni true story. For sure waweza kumuacha kwasababu ambayo inaweza ikufanye ujute sana kwa kumpoteza mtu akupendaye kwasababu kupata mtu akupendaye kwa dhati ni kazi ngumu sana hasa katika umri ambao mtu umekwisha rekebisha maisha kiasi fulani.