Mkuu kama unaenda kusoma kozi ambazo ukimaliza ili ufanye kazi vizuri tanzania ni lazima usajiriwe na bodi husika na kupewa leseni namaanisha kozi hasa za afya kozi kama medicine, pharmacy nk. Ni lazima upitie TCU wakupe kitu kinaitwa NO OBJECTION CERTIFICATE (noc certificate) ili ukimaliza na kurudi tz degree yako itambuliwe na kusajiriwa na bodi husika ya fani uliosomea kwa ajili ya leseni kwani hawatafanya hivyo bila degree yako kuwa-recognized na TCU sababu umesoma nje ya nchi.
Na ili hao TCU wakupe NOC CERTIFICATE ni lazima uwe umemeet minimum qualifications za kusoma kozi husika otherwise hawakupi.
So kuwa makini usije jikuta umefanya kazi bure na kupoteza muda na pesa bure.