Msaada wa kupata investors wa biashara

Masalu Jacob

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2017
Posts
1,013
Reaction score
1,183
Habari za muda huu.
Napenda kuomba kusaidiwa kwa yule mwenye ufahamu au kujua ni wapi naweza kupata muwekezaji mtu binafsi au kampuni.
Kwa yule ambaye anaweza kunisaidia nitashukuru sana.
Nitaomba anitumie aidha anwani ya barau pepe au tovuti PM ya wanaohusika na uwekezaji.
Shukrani sana
Mungu awabariki
 
Nadhani ungetanabaisha ni muwekezaji wa aina gani unataka yani sector ipi ili iwe rahisi kwa hao uliowashukuru in advance.
 
Nadhani ungetanabaisha ni muwekezaji wa aina gani unataka yani sector ipi ili iwe rahisi kwa hao uliowashukuru in advance.
Kwasasa nahitaji kwenye sekta ya viwanda hususani utengenezaji wa bidhaa (manufacturing industry).
Asante.
 
Its very hard kupata mwekezaji na its very easy kupata mwekezaji

iko hivi unategemea unataka kupata mwekezaji wa biashara ipi na sekta ipi...

Watanzania wengi kinachotushinda ni jinsi ya kuji present na jinsi ya ku present idea zetu wawekezaji wapo humu humu jamii forums kuna watu wana 700 millions humu kwenye accounts unakutana nao tu kariakoo

hawajui wapeleke wapi fedha zao wakikutana na wajanja wakawadanganya ndio wanawekeza kwenye biashara ambazo sio promising na wewe mwenye biashara ambayo nu promising inakufa

nikushauri kitu

Andika aina ya biashara yako
ikiwezekana weka na business plan humu kabisa watu waisome itawavutia hiyo kingine ongezea na check list kama Brela, acount ya biashara, board of directors, memorandum yaani vitu vyote ambavyo unaambatanisha ukienda bank kuomba mkopo wewe weka hapa yaani fungua uzi mwingine wa kuweka idea hiyo
kingine weka website na ofisi uonekane kidogo uko serious

Kwa kifupi anzisha biashara utafute mwekezaji wanapatikana nimeshuhudia

fedha ya investor inakuwa ni working capital

sasa wewe uko nyumbani unaangalia shilawadu hnasema tu unataka muwekezaji

endelea kumsubiri
 
 
 
Habari.
Mimi nina mpango wa biashara (business plan) nahitaji mwekezaji ambaye atanipatia mkopo wa $ 700,000 nataka kuwekeza kwenye mradi wa kutengeneza nguo namaanisha (Clothing line production). Tutaingia nae makubaiano kuwa faida itakayopatikana kwa mwaka nitampa 20% (profit sharing per yearly) na nitarejesha mtaji wake ndani ya miaka 10 au chini ya hapo.
Nimefanya utafiti kuhusu hii biashara kwani inasoko kubwa nchini na hata nje ya nje.
Kuhusu ni nguo gani zitazalishwa nimezianisha ndani ya mpango wa kibiashara ( business plan).
Kwa ambaye yupo tayari na anania njema ya kunifanya niweze kutengeneza hicho kiwanda namkaribisha aje anisaidie kwa kunipatia fedha, kuniunganisha na mwekezaji binafsi au mwekezaji kampuni.
Hii business plan inasema return kwa mm waka ni $ 500,000. Ina maana hata ndani ya miaka 5 naweza kurejesha fedha pamoja na hiyo riba ya 20%.
Shukrani sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…