TAI DUME
JF-Expert Member
- Feb 20, 2014
- 9,748
- 26,238
Wakuu habari ya mihangaiko
Ni kwamba nimekuwa nikiota nipo uwanjani nacheza mpira (football). Inaweza ikawa katika nafasi tofauti tofauti ila mara nyingi nacheza forward. Kinachonikwaza/Kushangaza katika ndoto hizo ni pale ninaposhindwa kutumia nafasi muhimu, let say kumalizia tuu kufunga goli. Yaani nakuwa najiposition vizuri, naomba pasi ya mwisho, napewa hiyo pasi ambapo kila mtu anategea nitafunga goli.
Kinachotokea sasa, miguu inakuwa mizito, siwezi kuukuta ule mpira, au hata nikiukuta huo mpira napiga kijishuti ambacho hakina madhara kabisa, Au naweza nikawa kwenye nafasi ya kutoa pasi ya mwisho, yaani mwenzangu anakuwa anasubiri tuu nimwekee pasi afunge, lakini utakuta siwezi kuufikia ule mpira au nikitoa pasi basi inapotelea kwa adui,
Usiku wa kuamkia leo imekuwa kiboko. Kwanza nilianza kucheza beki, yaani nilishindwa kuutoa golini mpira ambao nilikuwa kwenye nafas kubwa ya kuokoa goli. Nikasema nibadili namba nikaenda kucheza namba tisa. Basi nikapewa pasi ambayo ilikuwa ni ya kutupia tuu mpira golini, asee nilitoa boko ambalo kila mtu alishika kichwa, maana mpira niliugusa kwa tabu sana na haukwenda popote.
Ndoto za namna hii zimekuwa zikijirudia mara kwa mara. Sio muumini sana wa kuamini katika ndoto maana nilielezwa ni imaginations tuu za mtu anazowaza sana mchanana zinaweza zikajirudia kwa mtindo wa ndoto. Ila hii sasa imekuwa too much maana simalizi miezi miwili lazima nitaota mara mbili au tatu mfululizo,
Hii hali nimeanza kuiona huu ni kama mwaka wa pili sasa. By the way kwenye maisha yangu halisi mimi ni footballer mzuri tuu si wa kushindwa kufunga kwa nafasi kama zile.
Nimeanza kuhofia hii hali kwakweli.
WAZEE WA KUTAFSIRI HIZI MAMBO, MSAADA TAFADHALI