Msaada wa Lodge nzuri ya kufikia Mwanza Mjini

Nenda anoxa hotel jiran na uwanja wa furaisha, villa park, rock city mall unaenda kwa miguu. Bei ni ndogo sana elf 25 tu unapata breakfast ya buffet mpaka unasaza, unafuliwa na kunyooshewa nguo free hata kama begi zima
 
Tuelekeze ili wapi?
Njia panda ya mwaloni pale unaingia kulia mita Kama 30 tu Bei nakumbuka Ni kuanzia 25-40 Ni nzuri pia Kuna la Liga ipo nyasaka hutajutia Bei 25-30 Ni executive pia Kuna moja ipo kiloleli full ac 25, feni 20 Safi full huduma.
Angalizo Mwanza so far ni ipo loaded Kuna Mambo mengi yanaendelea in case unakuja Oda mapema ugeni mkubwa Hadi 13 Dec Ni mkubwa kitaifa ukimwi day, shimiwi, 40 ya son wa cdf, 9 Dec and son on and so forth
 
40 ya mtoto wa cdf....cdf ndo nan na inafanyika lini?
 
Ni pazuri sana afu asubuhi unapata breakfast ina supu pamoja na matunda mchanganyiko kwa 35,000/= tu, mwaka huu tena nilipita hapo nikakuta wanapafanyia marekebisho
Of course pazuri....labda wanataka wapafanyie marekebisho...
 
Mkuu uzuri unatofautiana, upi unaoutaka
 
Usihangaike sana victoria lodge ndio ipo katika kbs ya jiji na bei ni ya kawaida na ukiwa hapo ofc zote za serikal kufika ni rahic sana kuliko huko nyegezi inakuwa mbali na mji
 
Ipo sehemu gani hii?
Ni pembezoni mwa ziwa victoria, maeneo ya kamanga ferry!! Ukiwa town centre kwa boda boda ni buku jero tu. Vile vile kuna daladala, nadhani zinazotoka capripoint zinapita hapo!! Bwana hutajutia kuwa hapo!!ukishazoea hata kwa miguu unakwenda tu, unakuja hadi nyamagana stadium, unashuka hadi kamanga ferry, unafuata barababa inayokwenda kushoto unapanda nayo tu, pembezoni mwa ziwa, kama mita mia mkono wako wa kulia utaiona ipo kwenye mawe mawe!!
 
Sayi guest iko katikati ya mji,pale uhuru
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…