Habarini wadau
Kama kichwa cha habari kinavyosema, naombeni wale wajuzi katika lugha za kitaa wanisaidie kujua baadhi ya maana za maneno haya
1. Eneka
2. Kiki
3. Vizinga
4. Odah!
5. Kinyama, nk.
Na mengineyo unaweza kuongeza, ili wote tunaopenda lugha za kitaa tuzimudu vizuri. Santeni.
Sent using Jamii Forums mobile app
Oky,najua ila hata nji una mitaa so, kilichktakiwa ni misamiati ya simo/misimu ya vijanaMimi nipo mjini mkuu, sipo mtaani
[emoji120] [emoji120] sante sana mkuu1. Kiki - ni tabia ya mtu kupenda sifa au kutaka aonekane yuko juu au kujipa hadhi
2. Vizinga - Ni zile tabia za mtu kumuomba mwenziwe kitu sana sana hela, mfano umekutana na rafiki uako ambae muda mrefu hamjaonana, sasa katika maonhezi akakushtukiza na kukuomba hela.
3. Kinyama - Hutumika kama kielezi/kivumishi kinachoelezea muda mrefusana
Sent using Jamii Forums mobile app
Maneno haya mengine pia yanahitaji msaada 1. Ligi
2. Msembwende
3. Mbwembwe - majivuno au majisifu
4. Wenge - mapepe
5. Kishenzi - kielezi cha kusifia sawa na sana
6. Kishua - kielezi cha ambae kwao kuna uwezo
Sent using Jamii Forums mobile app