Msaada wa Macho.

Msaada wa Macho.

schneider

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2015
Posts
770
Reaction score
641
Habari za majukumu wakuu wenye ujuzi wa afya na wenye matatizo ya afya pia.

Kama kilivyo kichwa cha habari nasumbuliwa na macho kwa miaka mingi sasa na tatizo kubwa ni kuwa na macho mekundu ilo si kubwa sana kwa sababu naishi mijini labda niisiwe bangi.

Kubwa kabisa mara nyingi yanawasha na kutoa machozi kuna kipindi mwanga wa ghafla machozi yananitoka kwa wengi na kwa muda mrefu pia kuna kipindi ilikuwa nikianza kutizama tv tu kwanza yatoke machozi nikisha yafuta ndio niendelee na kuangalia.

Naomba msaada ndugu zanguni natanguliza shukrani nyingi sana.
 
wale wa kukaa muda mrefu wanacheza gemu kwenye kompyuta wanakutwa sana na haya mambo.
Na wale wanaonunua miwani mitaani na kuvaa tu kama fashion wakidhani ni urembo au wapendeze kumbe wanaharibu macho.

punguza kuona tv, pc na hata simu usiitumie gizani.

msosi mkuu, matunda, machungwa, mapapai, maembe kwa sana, maji mengi.
usiku lala muda wa kutosha, angalau sa5 uwe ushalala, ukifanya hivyo wiki hata 2 tu, utaona mabadiliko.
 
Back
Top Bottom