Katlesi Za Samaki
VIPIMO
Viazi 5 kiasi
Tuna 2 vikopo
Carrot 1
Pilipili mboga Nusu
Thomu ½ kijiko cha chai
Pilipili kiasi
Chumvi kiasi
Ndimu kiasi
Unga wa ngano ½ kikombe
Yai 1
Mafuta ya kupikia Kiasi
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
1.Menya Viazi uvichemshe na chumvi.
2.Vikiwiva vichuje maji, viponde ponde, vilainikie weka kando
3.Chuna carrot ziwe kama chicha, kata pilipili mboga nyembamba nyembamba, fungua vibati vya Tuna kamua majia yake mwaga.
4.Changanya Tuna, carrot, pilipili mboga, thomu, pilipili kali, chumvi, ndimu, kisha uchanganye na viazi ulivyoviponda. Hakikisha vimechanganyika vizuri.
5.Tengeneza vidonge kiasi unachotaka na kata umbo unalopenda kama la yai au duwara ukimaliza weka pembeni.
6.Changanya unga na maji uwe mzito mzito tena uchanganye vizuri na yai.
7.Weka karai katika moto, mimina mafuta kama ya maandazi, kisha chukua vidonge chovya katika unga uliochanganywa yai na utumbukize ndani ya mafuta yaliopashika moto vizuri.
8.Ziwache mpaka zibadilike rangu, uzitoe. Tayari kwa kula.
Katelesi Za Nyama
Vipimo:
Viazi 3 LB
Nyama 1 LB
Unga wa mkate (Breadcrumbs) 1 kikombe cha chai
Mayai 2-3
Mafuta ya kukaangia kiasi
Vipimo Vya Nyama:
Tangawazi mbichi na thomu iliyosagwa 1 kijiko cha supu
Chumvi Kiasi
Jeera (Bizari ya pilau ya unga) 1 kijiko cha chai
Dania (Gilgilani ya unga) 1 kijiko cha chai
Pilipili manga ya unga 1 kijiko cha chai
Mdalasini wa unga ¼ kijiko cha chai
Pilipili mbichi iliyosagwa 1 kijiko cha chai
Ndimu au limau 2 vijiko vya supu
Kotmiri iliyokatwakatwa (chopped) ½ kikombe cha chai
Kitunguu kilichokatwa katwa (chopped) 1 Kikubwa
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
1.Chemsha Viazi, vikiwiva menya maganda na viponde.
2.Weka nyama katika sufuria ndogo, ichanganye na vitu vyake vyote isipokuwa kotmiri na vitunguu.
3.Ipike nyama mpaka ikauke.
4.Tia Kotmiri na vitunguu viliyokatwakatwa, changanya weka kando.
5.Chukua viazi viliyopondwa Changanya na hiyo nyama.
6.Fanya madonge kiasi katika mkono ufanye viduara.
7.Tayarisha katlesi zote hivyo hadi umalize viazi na nyama.
8.Weka mafuta katika karai yapate moto sawa sawa.
9.Chomva katlesi katika mayai uliyoyapiga sawa sawa kisha garagaza katika unga wa mkate (breadcrumbs) na uzikaange mpaka zigeuke rangi.
10.Epua weka katika karatasi ya inayokunwa mafuta (Kitchen paper) au weka katika chujio zichuje mafuta. Tayari kuliwa.