Kajabila
JF-Expert Member
- Jan 7, 2017
- 539
- 942
Wakuu habari!! Mwenzenu kuna Boss kanifungulia kesi ya kumwibia hela ofisini kwake kitu ambacho si kweli kwani mimi siko ofisini toka mwezi wa 4. Ilikuwa hivi nilkua nafanya kazi katika taasisi fulani hivi ya kifedha nilifanya kazi pale bila ata mkataba wala malipo yanayo eleweka. Na ofisini tulikuwa watatu mimi na wenzangu Boss alianza kusumbua maneno maneno mimi nikaona hapa hakuna kazi nikimpigia simu kwani hakuwepo kumjulisha kuacha kazi akakubali akaniuliza kuhusu hesabu nikamwambia nmikabidhi kwa walio baki basi tukakubaliana nikaacha toka huo mwezi wa 4 atukuwai kuwasiliana tena mpaka juzi mwezi 10 alipo kuja na police eti nimemwibia millioni 15 pamoja na wale wenzangu nilio waacha. Police kasema mimi nimeiba hela zake kuna mahali nilipo kuwa ofisi tulikua tunachukua hela za kufanyia kazi ofisini na pale mahali tulikuwa tunasign tukichukua ndo kawaleta hao kama mashahidi. Nilipo kuwa ofisi kila nikichukua hela kwa hao watu nilkua na mtumia na maelezo yote ninayo kwenye simu yangu yeye kadai nilkuwa nikichukua sifikishi ofisini kitu ambacho si kweli na hizo hela yeye ndo alkua anazitumia kwa matumizi yake binafsi na idadi ya matumizi ninayo. Na kila siku nilkua natuma report ya ofisini na uwezi kuondoka kama hesabu haziko vizuri. Na Boss yeye ataki kwenda mahakamani anataka kuishia police eti tumlipe hela zake na yeye hana ushahidi wa document alizo ingia hiyo hasara. Naombeni msaada kwenye hili ndugu zangu na maswali ya kuwauliza mashahidi