Msaada wa mawazo katika hili

jokotinda_Jr

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2022
Posts
882
Reaction score
1,536
Msaada tutani .... ipi nafasi ya mdhamini ikiwa kesi itafikishwa mahakamani ......... yaani ikiwa mmi nime mdhamini na mlalamikaji akasema kesi iende mahakamani mimi kama mdhamini wa mtuhumiwa natakiwa nifanyeje .... msaada tafadhali
 
Ulimdhamini polisi? Kama Ni hivo Hapo udhamini wako ushaisha kesi ikifika mahakamani unatakiwa kumdhamini upya Kama unataka kuendelea kumdhaminj
 
Yes nilimdhamini polisi na mlalamikaji ameomba kesi ifikishwe mahakamani ndo nataka kufahamu nikifika mahakamani nafasi yangu itakuwa ipi
 
Ulimdhamini polisi? Kama Ni hivo Hapo udhamini wako ushaisha kesi ikifika mahakamani unatakiwa kumdhamini upya Kama unataka kuendelea kumdhaminj
Maana yule askari amenipigia simu amesema kesho niripoti kituoni yule mlalamikaji ameomba kesi ipelekwe mahakamani
 
Hapo inachotakiwa Ni Wew ufike na mtuhumiwa Hapo kituoni Ila mngeangalia Ni namna gani mmalizane nje ya mahakama
 
Muulize kesi inaenda mahakama ipi ili uandae documents ukamdhamini tena mahakamani
 
Hapo inachotakiwa Ni Wew ufike na mtuhumiwa Hapo kituoni Ila mngeangalia Ni namna gani mmalizane nje ya mahakama
Ikowa mlalamikaji atagoma maongezi na kesi ikafika mahakamani nni kitanipata mmi
 
Msaada tutani .... ipi nafasi ya mdhamini ikiwa kesi itafikishwa mahakamani ......... yaani ikiwa mmi nime mdhamini na mlalamikaji akasema kesi iende mahakamani mimi kama mdhamini wa mtuhumiwa natakiwa nifanyeje .... msaada tafadhali
Unatakiwa kutekeleza masharti ya dhamana kwa kuhakikisha anafika kituoni au mahakamani kwa siku na tarehe iliyopangwa bila kukosa na kama kuna dharura inatakiwa utoe taarifa mapema juu ya mshtakiwa uliyemdhamini ili usije ukakamatwa au kushtakiwa badala yake au mali uliyoweka dhamana kutaifishwa sababu ya mshtakiwa kuruka dhamana
 
Hapo inachotakiwa Ni Wew ufike na mtuhumiwa Hapo kituoni Ila mngeangalia Ni namna gani mmalizane nje ya mahakama
sasa kama mshtakiwa haoni sababu ya kumalizana na mlalamikaji kwa nini mdhamini ateseke?
 
Mdhamini kazi yako kuhakikisha mtuhumiwa anakuwapo kipindi chote cha kesi inavyoendeshwa.

Ama kama kapata udhuru au ugonjwa basi lazima uwepo kutoa taarifa mapema.

Endapo mtuhumiwa akatoroka kipindi cha kesi, basi utalazimika wewe kukaa rumande mpaka pale mtuhumiwa atakapopatikana.

Unaweza kudhamini kama unamuamini mtu na unajua mienendo yake kwamba hatatoroka.

Muda mwingine, endapo dhamana uliweka kitu fulani na mtuhumiwa kupotea, basi mahakama itaitaifisha mali husika kama hutompata mtuhumiwa.
 
Msaada tutani .... ipi nafasi ya mdhamini ikiwa kesi itafikishwa mahakamani ......... yaani ikiwa mmi nime mdhamini na mlalamikaji akasema kesi iende mahakamani mimi kama mdhamini wa mtuhumiwa natakiwa nifanyeje .... msaada tafadhali
nafasi yako kama mdhamini katika dhamana ya polisi inayotokewa na polisi inakuwa imeishia hapo. Nahautakuwa tena mdhamini wake kwa upande wa mahakamani labda ukimdhamini tena mahakamani.

status yako hapo unakuwa si mdhamini tena na dhamana ya polisi inakoma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…