Msaada wa mawazo kuhusu hisa au kuhifadhi dola zangu

Msaada wa mawazo kuhusu hisa au kuhifadhi dola zangu

mwasambili

Senior Member
Joined
Oct 28, 2013
Posts
151
Reaction score
77
Heshima kwenu ndugu zangu,,
nimiaka mitano sasa nilihifadhi dola 200 za marekani,sasa nilipata elimu kidogo juu ya hisa(haikunitosheleza),sasa naomba ushauri nizibadishe hizi fedha kuwa za kitanzania halafu ninunue hisa 300 katika benki ya mkombozi au niendelee kuzitunza?,kwani kwa sasa hawa mkombozi wanauza hisa moja Tsh1000,na kila anaechukua aanzie na hisa 100,na tafadhali kwa baada ya miaka miwili hadi mitani naweza kufaidika vipi.
natanguliza shukrani na Mungu azidi kuwapa uhai
 
Dola 200 baada ya kuzitunza Zilizaa? Duh kweli ukisikia maajabu ndio haya!!!
 
Dola 200 baada ya kuzitunza Zilizaa? Duh kweli ukisikia maajabu ndio haya!!!

Zimezaa ndio! Maajabu yako wapi? Unajua exchange rate ya miaka mitano nyuma ilikuwaje? Na sasa ikoje? Inflation je?

Kiufupi jamaa ametunza value ya pesa yake vizuri kwa sababu dollar ina appreciate wakati shilingi yetu ina depreciate kila leo.
 
Mkuu kwenye hisa inabidi uwe makini kidogo. Misingi ya uwekezaji inasema hivi " wakeza kiasi cha pesa ambacho uko tayari kukipoteza ikitokea jambo lolote"

Kwenye stock exchange risk ni kubwa sana. Kwani hakuna uhakika kwamba hisa zita fanya vizuri mara baada ya kuanza kuuzwa sokoni. Japokuwa kuna viashiria vinavyoweza kukuonesha future performance ya shares; mfano. Historical profit, strength ya balance sheet, healthy ya cash flow etc
Shida nyingine ni kwamba DSE sio liquid kivile, sometimes inaleta shida pale mtu unapotaka ku exit.
Heshima kwenu ndugu zangu,,
nimiaka mitano sasa nilihifadhi dola 200 za marekani,sasa nilipata elimu kidogo juu ya hisa(haikunitosheleza),sasa naomba ushauri nizibadishe hizi fedha kuwa za kitanzania halafu ninunue hisa 300 katika benki ya mkombozi au niendelee kuzitunza?,kwani kwa sasa hawa mkombozi wanauza hisa moja Tsh1000,na kila anaechukua aanzie na hisa 100,na tafadhali kwa baada ya miaka miwili hadi mitani naweza kufaidika vipi.
natanguliza shukrani na Mungu azidi kuwapa uhai
 
Eti unajua thamani ya Dola miaka 5 iliyopita!!!!!!,mshauri basi aendelee kuitunza hiyo dola 200 itafika Bilioni.
 
Back
Top Bottom