Msaada wa mawazo: Nataka kuanza kilimo cha maharage

Bhahebhu

Member
Joined
Dec 3, 2021
Posts
36
Reaction score
43
Wakuu nawasalimu,

Heri ya sikukukuu ya Pasaka. Kama kichwa cha habari kinavyojieleza naomba msaada nataka kuanza kilimo cha maharage na target yangu ni kupata gunia zisizopungua 100, naomba kusaidiwa ni hekali ngapi zitanifikisha katika hyo target?

Palizi yake ni mara ngap, mavuno ni baada ya miezi mingapi, na soko lake lipoje hasa hapa Tanzania. 🙏🙏
 
Ninavyojua maharage mpaka kuvuna ni miezi minne au mitano coz utasubiri yakaukie shambani.

Palizi huwa mbili au tatu ndugu, wengine watamalizia hizo idadi za heka na magunia unayotarajia kuyavuna.

Kila la heri kwako...!
 
Maharage ukilima vizuri palizi n moja hadi mbili...
Hutumia siku 70-85 kukomaa...
Kwa ardhi nzuri unahitaji hekari 15 ili kupata gunia 100 za kilo 100... Ikiwa wastani wa gunia 6.5 kwa hekari
 
Best soil ni debr 32 kwa heka. Mbegu debe mbili mbolea ya kuku inafanya vizuri zaidi.
 
Wakuu salaam, na mimi pia napanga kulima maharage msimu huu wa kilimo. Sasa swali langu ni je, naweza kupanda maharage kwenye shamba la mahindi? Yaani mahindi nikapanda mwezi huu wa kumi na mbili alafu nikaja kupanda maharage kwenye shamba hilo hilo mwezi wa tatu? Kipindi tayari mahindi yamshakua? Naombeni muongozo wenu wazoefu maana isije nikajichanganya.
 
Shamba lipo mkoa gani?
 
Ni mkoa upi unalima maharage kwa uzuri kabisa hasa haya ya njano?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…