Mkuu, "kila kinachong'ara sio dhahabu".
Kama umeridhika na mpenzi wako wa sasa hivi wewe endelea na kumuheshimu huyo dada na jaribu pia kuepusha mazungumzo ya kumuonesha kwamba na wewe pia uko available.
Kutamani ni sehemu ya uanaume na kuweza ku-control matamanio ni uanaume pia. Kuna wakina dada warembo wengi sana na wote wanakuja kwa tabia tofauti, nzuri na mbaya. Sasa tutawatamani na kuwataka wangapi?
Kama una furaha na mpenzi wako wa sasa hivi basi nakushauri usiipoteza hio furaha kwani huna huakika huyu unayemtamani atakuja na full package. Sasa kwanini u-risk kumpoteza huyu wa sasa hivi ambaye upo nae na ujataja matatizo yoyote?
Na ukimpata huyu wa sasa hivi unaye mtamani,je ukimuona mwingine ukamtani nae itakuwaje? Ndio maana nikasema hapo juu,kuweza ku-control matamanio ni sehemu ya uanaume pia.
Nina huakika huna nia ya kuwachezea hawa wadada wawili, kama una nia hio sidhani kama ungekuja kuomba ushauri hapa mkuu.
Huo ndio ushauri wangu mkuu.
Kila la kheri.