Msaada wa mawazo

ossy

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2011
Posts
872
Reaction score
143
wakuu heshima yenu....naombeni tafsiri ya majibu yangu baada ya kufanya kipimo cha sperm analysis....ninampango wa kupeleka kwa daktari na shemeji yenu but nataka nijue nini maana ya haya majibu kabla ya mtu mwingine yeyote...na nini maana yake? Asanteni...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza ni kitu gani kimekusukuma kufanya hiki kipimo?
 
Mkuu kwanza nikupongeze kwa kwenda kufanya kipimo cha sperm analysis ili kuweza kujua kama una uwezo wa kutoa mbegu ambazo zitaweza kumpa mwanamke mimba..... Hicho kipimo kwanza kinatusaidia kujua idadi ya mbegu katika bao moja na pia ubora wa mbegu katika uwo mkojoo mmoja....

Kutoka na majibu yako hapo kwa karatasi nianze kufafanua parameter moja moja.....

1. Volume- Kutokana na majibu yako hapo inaonesha wazi unatoa kiwango kidogo cha shahawa amabacho ni 0.6mls ukilinganisha na 1.5mls ambacho mtu anatakiwa kutoa (tatizo)

2. pH- PH ya shahawa yako iko chini yaani ni acidic kwa maana nyingine hii pia huchangia kuua mbegu za kiume na pia hata zisipokufa zinathiri ufanyaji kazi wake katika kurutubisha yai. (tatizo)

3. Color- iko safi haina tatizo

4.Liquefection- kuna tatizo kwa kawaida liquefection time ni dakika 20-30 juu ya hapo kuna tatizo

5. Sperm count/ml - Hawakuweza kuona hata sperm moja ikitembea kwa shahawa and kutokana na majibu yako hapo naona NIL hii inamaanisha yaani ni sifuri na majibu yakileta nil mara nyingi inaweza kuwa ulihasiwa mkuu (tatizo) but kwa kawaida 1ml of semen inatakiwa iwe na more than 20 million spermatozoa

HITIMISHO

Mkuu inaonesha wazi una tatizo la uzazi na kwa hali hiyo ya majibu katika karatasi yako yaonesha huna uwezo wa kumpa mwanamke ujazito (infertility ) pole sana mkuuu
 
Daa kaka huu uchambuzi wako umenifanya mpaka nimekuna kichwa.

Kaka mhusika pole sana ndugu yangu labda mkuu atusaidie hamna njia jamaa anaweza akafanya kuponywa tatizo lake mkuu.
 
Asante mkuu.....je tatizo linaweza kuwa ni nini? je na kama ujanani nilipata mtoto hii inajuwaje? coz nina mtoto mmoja ambaye nilipata ujanani na nina uhakika ni wangu sababu anafanana na mimi kila kitu!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante mkuu.....je tatizo linaweza kuwa ni nini? je na kama ujanani nilipata mtoto hii inajuwaje? coz nina mtoto mmoja ambaye nilipata ujanani na nina uhakika ni wangu sababu anafanana na mimi kila kitu!


Sent using Jamii Forums mobile app

Twende mojamoja katika mada... kwa kitaalamu tatizo lako linaingia katika kundi hili linaloitwa " Impotentia generandii" ambayo humaanisha ya kwamba unauwezo wa kupiga kazi vizuri kabisa bila tatizo but kile unachokitoa (semen) hazina uwezo wa kurutubisha Yai ili kuweza kutengeneza kijusi.

Hivyo basi kuna vitu mbalimbali ambavyo huweza kupelekea tatizo la Impotentia generandii kuweza kutokea kama nitakavyoelezea hapa chini;

  1. Congenital and Medical causes kama vile;
  • Infection kama vile orchitis and epididymitis ambayo ni inflammation/muwasho wa korodani na mirija inayosafirisha mbegu (epididymis) ambapo pia muwasho huo waweza hatarisha uzalishaji wa mbegu na pia huweza pelekea hiyo mirija kuziba na hivyo kupelekea tatizo pia magonjwa mengine ya zinaaa kama vile gonorrhea huweza hatarisha uzalishaji wa mbegu pia.
  • Varicocele Hili tatizo hutokana na kuvimba kwa mishipa ya vein na artery ambayo husafirisha damu katika eneo la korodani na hivyo hupelekea kutokuruhusu kiwango maalum cha damu kufika katika korodani na hivyo kuathiri uzalishaji na uquality wa mbegu.
  • Chromosome defects Kama vile Klinefelter's syndrome,Kallmann's syndrome na Kartagener's syndrome ambapo mwanaume huzaliwa na XX-Y chromosome badala ya X-Y chromososme ambapo hupelekea matatizo katika maungo ya kiume but kwa hili sidhani kama ni tatizo kwako.
  • Hormone Imbalance ambapo husababishwa na tatizo katika korodani au mfumo mzima wa hormone kama vile Hypothalamus, pituitary.thyroid and adrenal gland ambapo huathiri mfumo mzima wa uzalishaji wa Testosterone Hormone ambayo hutumika katika kuzalisha mbegu za kiume.
  • Matumizi ya muda mrefu wa madawa kama vile steroid drugs, anti-ulcer therapy, anti-fungal drugs and cancer medication (chemotherapy) pia yaweza kuathiri mfumo mzima wa uzalishaji wa mbegu katika korodani.
  • Matumizi ya muda mrefu ya X-rays pia yaweza sababisha uzalishaji wa mbegu kuwa katika kiwango kidog0

2. Healthy and lifestyle factors
  • Hapa nazungumzia unywaji wa pombe na uvutaji wa sigara kupita kiasi pia yaweza kuwa tatizo kwani hupelekea kupungua kwa uzalishwaji wa Testosterone Hormone ambayo hutumika katika uzalishaji wa mbegu
  • Pia stress za muda mrefu hupelekea tatizo la uzalishaji wa mbegu kuwa duni kwani huathiri pia mfumo mzima wa hormone kama nilivyokwisha elezea hapo mwanzo.
HITIMISHO

Katika scenario ya wewe kuwa na mtoto siwezi kataa mkuu.... labda kwa kipindi hicho ulikuwa na uwezo wa kuweza kumpa mwanamke ujazito and tatizo halikuwa sugu sana kama ilivyo kwa sasa....

My intake unaweza enda Hospitali kwa vipimo zaidi ili kuweza kujua viwango vya Testosterone, Follicle stimulating Hormone (FSH), Lutenizing Hormone (LH) and Prolactin na pia wanaweza chukua kipimo cha Anti-sperm antibodies kwani kuna baadhi ya immune system cells za mwili zinaweza ku detect sperm kama moja wapo ya invader katika mwili na hivyo kupelekea sperms kuvamiwa na kuuliwa ni hayo tu mkuu.
 
dah...Asante sana mkuu.. kati ya hayo yote sinywi wala sivutii kabisa katika maisha yangu yote...je kwa uzoefu wako wa kitabibu kunauwezekano wa kupona kweli? Thanks

Sent using Jamii Forums mobile app
 
dah...Asante sana mkuu.. kati ya hayo yote sinywi wala sivutii kabisa katika maisha yangu yote...je kwa uzoefu wako wa kitabibu kunauwezekano wa kupona kweli? Thanks

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu inaweza kuwa Yes or No na hapo inategemea na nini yaweza kuwa tatizo la wewe kuwa na azoospermia ndio maana nimekuambia inakubidi urudi tena hospitali kwa vipimo zaidi ili kuweza ku identify tatizo hapo then ndio utaweza weza jua either unaweza pona or kutokupona tatizo lako Mkuu.

Tena umesema kabisa hapo mwanzo upo na mtoto maybe tatizo linaweza kuwa mishipa inayosafirisha sperms kutoka kwa kiwanda cha uzalishaji imeziba but hizo bado zaweza kuwa assumption kila la kheri mkuu....
 
pamoja sana mkuu....umekuwa msaada sana..Thanks alot

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…