habari wanajamvi.....hivi milioni 15 inaweza kufanikisha kujenga nyumba?
Kama umeshanunua kiwanja tayari fanya yafuatayo:
1 - Tafuta wachora ramani, wajenzi, wahandisi ama wadau katika masuala ya ujenzi wa nyumba, kisha waeleze aina ya nyumba unayoitaka kujenga ili kupata ushauri wa manunuzi ya vifaa, malipo ya ufundi, na gharama za ujenzi kamili kulingana na eneo husika na mwisho maliza na kuchora ramani ya hiyo nyumba.
2 - Fanya biashara hicho kiasi ulichonacho ili walau uweze kupata kiasi fulani cha fedha kutoka katika faida ya bishara hiyo / hizo kila mwezi ambapo itakuwa rahisi kwako kupeleka fedha hizo katika ujenzi wa nyumba yako na ukafanikiwa kujenga taratibu taratibu kuliko kusubiri kuwa na hela ya pamoja ndo ujenge nyumba. Aina ya biashara itegemee uwezo wako, ujuzi wako, uzoefu wako, elimu yako, ndoto zako, vitu unavyopenda, dini yako, umri wako, jinsia yako, watu wa karibu unaoishi nao, mtaji wako, na mengine kama hayo yanayohusika kwa namna moja ama nyingine katika hiyo biashara.