..msaada wa mawazo...

..msaada wa mawazo...

mymy

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2011
Posts
296
Reaction score
111
habari wanajamvi.....hivi milioni 15 inaweza kufanikisha kujenga nyumba?
 
habari wanajamvi.....hivi milioni 15 inaweza kufanikisha kujenga nyumba?
Ni vizuri ukaeleza walau unataka nyumba yako iweje ili ile rahisi kukusaidia, hata wapi unataka kuijenga hiyo nyumba yako ni muhimu pia
 
...asante dancan...eneo ni kibada ya kigamboni....nyumba ya vyumba vitano....
 
...asante dancan...eneo ni kibada ya kigamboni....nyumba ya vyumba vitano....

Nyumba ya vyumba 5 SIO NYUMBA NDOGO. hiyo ela yako HAITOSHI...
 
Ndugu pembejeo za ujenzi gharama kweli kipindi hiki hiyo hela haitoshi ukizingatia haliya kibada mi pia nimkazi huko.
 
...asante wadau kwa msaada wenu....
 
...asante wadau kwa msaada wenu....
Ila usikate tamaa maana nyumba haijengwi leo na kuhamia leo unaweza ukaanza kidogo kidogo mpaka itakapofika mwisho ndugu ili mradi uwe na kipato kinachoingia hata kama sio kikubwa sana, usizione hizo nyumba ukiuliza wngine wamejengaje unaweza kujiona wewe tajiri kwa maana ya kuanza na hela nyingi
 
habari wanajamvi.....hivi milioni 15 inaweza kufanikisha kujenga nyumba?

Kama umeshanunua kiwanja tayari fanya yafuatayo:
1 - Tafuta wachora ramani, wajenzi, wahandisi ama wadau katika masuala ya ujenzi wa nyumba, kisha waeleze aina ya nyumba unayoitaka kujenga ili kupata ushauri wa manunuzi ya vifaa, malipo ya ufundi, na gharama za ujenzi kamili kulingana na eneo husika na mwisho maliza na kuchora ramani ya hiyo nyumba.
2 - Fanya biashara hicho kiasi ulichonacho ili walau uweze kupata kiasi fulani cha fedha kutoka katika faida ya bishara hiyo / hizo kila mwezi ambapo itakuwa rahisi kwako kupeleka fedha hizo katika ujenzi wa nyumba yako na ukafanikiwa kujenga taratibu taratibu kuliko kusubiri kuwa na hela ya pamoja ndo ujenge nyumba. Aina ya biashara itegemee uwezo wako, ujuzi wako, uzoefu wako, elimu yako, ndoto zako, vitu unavyopenda, dini yako, umri wako, jinsia yako, watu wa karibu unaoishi nao, mtaji wako, na mengine kama hayo yanayohusika kwa namna moja ama nyingine katika hiyo biashara.
 
Kwa hiyo hela na hiyo nyumba unayoitaka! waweza jenga boma then ukaja malizia baadae ukijichanga tena
 
Back
Top Bottom