Msaada wa mchanganuo wa bei na miundombinu kuanzisha kituo cha mafuta (petrol station)

asanteni kwa ushauri wenu,nitaufanyia kazi pia kama mna zahidi la kuongea naomba mueendelee kushauri,kwani natumaini kuna watu wengine apa pia wangependa kujua,mbarikiwe
 

True mkuu, hilo ndo Tatizo na hii inasababishwa na UMIMI, kila mtu anaona bora amiliki DUKA, Unakuta mtaa unawakazi 400 kuna maduka 30 hapo ndo ujiulize,
Na kuanza na mazao ya kilimo na mifigo na vizuri kabisa, tena inatosha kabisa,
 
Mkuu usifanye biashara hizo. Hazina faida.
Ila kama una connections na hujali dhuluma, basi unaweza pata faida.

Mkuu ni biashara GANI isiyo kuwa na faida, chocote kinacho itwa biashara ni lazima iwe nafaida bila kujalisha ni kiasi gani cha FAIDA

Na hata hivyo ili kutengeneza FAIDA inategemena na huduma yako, make huduma ndo inadetermine FAIDA
 


Mkuu sahihisho kidogo. Shell ni kampuni ya mafuta kama ilivyo BP, PUMA, GAPCO n.k. Ukisema sheli ya Gapco ni sawasawa na kusema BP ya GAPCO.
 
Mkuu sahihisho kidogo. Shell ni kampuni ya mafuta kama ilivyo BP, PUMA, GAPCO n.k. Ukisema sheli ya Gapco ni sawasawa na kusema BP ya GAPCO.

Shell ni kati ya kampuni zilizoanza biashara hizi kwa hapa nchini filling station zote kibongo-bongo tulisummerrize kwa jina hilo shell..
 

Nimeupenda mtiririko wako jinsi ulivyojibu big up
 
Nakubaliana na hoja za baadhi ya wadau, mimi binafsi ni agent wa viwanja hasa hivyo vya sheli na supermarket na nimeona jinsi wanavyofanya. kuna namna 2 mosi ukiisha pata eneo unaweza waona kampuni mama ile ambayo ungependa uuze bidhaa yao . na wao watakujengea na kuweka pump ila visima unachimba kwa gharama zako. na kituo kikikamilika unatakiwa kudiposit $ 300,000 kwenye fixed account kwa muda fulani, ndipo wao watakuwa wanakupa mafuta na wewe unachukua commission kwa muda fulani hv. njia ya pili ni kujilipua kila kitu unanunua cha kwako na jina la kituo linakuwa la kwako
 
naomba kufahamu kama nshajenga kituo changu cha kuuzia mafuta, je natakiwa kuwa na vitu gani kabla ya kwenda ewura kupata leseni....cjui pa kuanzia jamani...msaada..munitajie vitu ntakavyokwenda navyo ewura....


Msaada jamani naona kama muda unakimbia napoteza muda.....
 
Reactions: SDG
Kuna aina mbili za hivyo vituo!aina kwanza jenga cha kwako....kwa standard ya (seek ushauri kwa Oilcom,Gapco,Total etc) ambao watakuuzia hayo mafuta!unakuwa unatumia logo yao .....ukishajenga kituo,unaweka deposit kwao mnaanza biashara!unaletewa mzigo ukiuza unapeleka hela yao ww unabakia faida....wanaleta tena!ila lazima uweke deposit kama 150m hivi!ama la uwe unanunua cash bin cash...hakuna kuchagua kampuni ya kukuuzia!unaenda popote na kununua mzigo unamwaga na kuuza!wajuzi zaidi wakiamka watakumwagia zaidi!subiri
 

sasa ili nianze ya kwangu mwenyewe nijenge na kununua na kuuza kwa business name yangu mwenyewe niwe na nini...natakiwa kuwa na nini b4 naenda kuomba leseni kule ewura? Nafikiri umenielewa mkuu
 
Reactions: SDG
Heshima yenu wakuu, msaaada mwenye kujua gharama za kufungua sheli ya mafuta, nataka nifanye hii biashara niko mkoani tatizo sijui pakuanzia wapi, mtaji sio tatizo, mwenye mchanganuo plz share,mbarikiwe sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…