Msaada wa mchanganuo wa bei na miundombinu kuanzisha kituo cha mafuta (petrol station)

Msaada wa mchanganuo wa bei na miundombinu kuanzisha kituo cha mafuta (petrol station)

yes ni kituo kilichokamilika ila chenye canopy ndogo za kwenye pump.
 
ina cover jengo dogo ambalo huwa ni kama ofisi na duka la vilainishi, matank madogo ya lita 10,000 matatu
 
Hongera kwa wazo zuri la kibiashara ila kuanzisha kituo kipya itakuchukua kama mwaka mzima hivi kuweza kukamilisha kila kitu hadi kufungua kituo.

hatua ya kwanza ni kupata eneo la kuweka kituo lililotengwa kwa ajili ya biashara hiyo, ya pili unatakiwa kwenda halmashauri kuomba kibali cha ujenzi, tatu utaenda Fire kupata certificate ya kujenga kituo, nne itakubidi ufanye Environmental impact assessment, ukishapata certificate unaenda Ewura kwa ajili ya vibali. baada hapo ndio unaweza kuanza kujenga kituo.

kuna watu huwa hawafuati hizo taratibu ila huwa kuna shida zake na hasa kwa kipindi hiki.

kujenga kituo standard ambacho hutopata shida ya ewura kwa kijijini ni kama 150m.
Nakubaliana na mkuu,ameelzea vizuri saana ubarikiwe kamanda
Kuna jamaa aliwahi kunipa figure kama hiyo.Maana nasikia kwa mwanzo mafuta unaweza kukopeshwa mpaka utakaposimama
 
Hongera kwa wazo zuri la kibiashara ila kuanzisha kituo kipya itakuchukua kama mwaka mzima hivi kuweza kukamilisha kila kitu hadi kufungua kituo.

hatua ya kwanza ni kupata eneo la kuweka kituo lililotengwa kwa ajili ya biashara hiyo, ya pili unatakiwa kwenda halmashauri kuomba kibali cha ujenzi, tatu utaenda Fire kupata certificate ya kujenga kituo, nne itakubidi ufanye Environmental impact assessment, ukishapata certificate unaenda Ewura kwa ajili ya vibali. baada hapo ndio unaweza kuanza kujenga kituo.

kuna watu huwa hawafuati hizo taratibu ila huwa kuna shida zake na hasa kwa kipindi hiki.

kujenga kituo standard ambacho hutopata shida ya ewura kwa kijijini ni kama 150m.

Mkuu ubarikiwe sana
 
Heshima yenu wakuu, msaada mwenye kujua ghalama za kufungua kituo cha kuuza mafua (filling station) nataka nifanye hii biashara nipo mkoani tatizo sijui pakuanzia wapi mtaji sio tatizo mwenye mchanganuo wa biashara hii plz share mbarikiwe sana
 
Nipigie 0756837183
 
Mwenye kujua hatua zakuanzisha filling station share nasi tuweze kuzijuwa
Maximum ya mtaji wakufungua filling station
 
Mkuu Pamoja na location ambayo kutoka na UFISADI haifuatwi kwa sasa, ila kuna mambo mengine

Zile kampuni za mafuta kama Total, Lake oil, BP, GAPCO na kazalika ukienda na Proposal ya kueleweka huwa wanakujengea na wewe unakua unauza tu mafuta na ukienda kinyume na Sheria zao wana kunyang'anya sheli mida hiyo hiyo hawana mchezo,

So kuna wanao jenga vya kwao wenyewe na kuna vya Makampuni, na vingi vyenye Majina ya watu binafisi au sehemu uje ni mtu mwenyewe kajenga, Mfano JUMA PETRO STATION, SERENGETI FILLING STATION, hivi huwa ni vya watu binafsi, ila vile vyote vyenye majina ya Makampuni kama vile TOTAL, GAPCO, CAMEL. LAKE OIL, BP, na vinginevyo hizi vimejengwa na wenye makampuni na wanao uza ni menegment tu na mwisho wa siku wanakulipa kamisheni ya kuuza, na hapa kama Sheli ni ya GAPCO ukiuza mafuta ya TOTAL inakula kwako mazima, NA UNALAZIMIKA KUUZA NA GRESE ZAO, OIL ZOTE MBILI NA MAFUTA YA BREAK YA KAMPUNI YAO

Ila kama sheli umejenga wewe mwenyewe una mamlaka ya kuuza mafuta ya kampuni yeyote ile iwe SPACE OIL, LAKE OIL NA KAZALIKA,

ISHU ZA KUWEKA SUPEMARKET NI MANJONJO YA WEWE ULIE PEWA JUKUMU LA KUUZA MAFUTA, ILA KISHERIA BADO NI HATARI INGAWA WAPO WANAO WEKA HADI GEST SHELI
Swali la nyongeza kaka,

Tuchukulie nimefungua kituo cha uuzaji mafuta, na gharama zote hadi ufunguzi wa kamouni ni juu yangu.

Kwa maana hio, kituo kikaitwa kwa jina langu!

Swali langu ni ;

Mafuta nitakua nanunua wapi na kuleta kwenye visima vya kituo changu.?!

Na bei za jumla ni kiasi gani.?!
 
Ukiacha mawazo mazuri kutoka humu JF , bado ushauri wangu MWEKEZAJI yeyote aliye serious na yuko tayari kutumia rasilimali zake, basi ni vema akapenda kutumia washauri waelekezi wafanye planning nzuri itakayo zaa Business Plan nzuri. Nina uhakika maswali yatakuwa machache. Tatizo wengi tunakimbia huduma za Consultants, tunaegemea ushauri wa jumla kutoka kwa wzoefu na wajuaji. (japo ni good source...ila sio ya kutegemea).
 
Naomba kujua pump za mafuta zinauzwaje na yale matank ya mafuta yanatengenezwa wapi,?
 
Mkuu naomba mrejesho wa hii kitu...
umefanikiwa maana na mimi nataka nijikite kwenye biashara husika.
Thanks in advance.
 
Mkuu naomba mrejesho wa hii kitu...
umefanikiwa maana na mimi nataka nijikite kwenye biashara husika.
Thanks in advance.
Mkuu, binafsi nilikwenda GAPCO wakati wa maonyesho ya sabasaba (walikuwa na banda), walinikaribisha vema. Baada ya maongezi mafupi walinialika kufika ofisini kwao. Cha msingi walitaka kujua kama ninamiliki eneo ambalo ni potential, halafu kama nina vifaa. Nikawaambia mimi nina eneo tu, wakasema vingine watatoa wao.

Bahati mbaya baada ya maonesho nilisafiri kwa zaidi ya mwaka, niliporudi sikuwa na msukumo tena. Ila nakiri jamaa walikuwa tayari kusaidia na walihitaji sana.
 
Asante mkuu kwa jibu zuri...
je inawezekana nikaanzisha yangu bila kupitia kwa hao mabwana?
 
naomba kufahamu kama nshajenga kituo changu cha kuuzia mafuta, je natakiwa kuwa na vitu gani kabla ya kwenda ewura kupata leseni....cjui pa kuanzia jamani...msaada..munitajie vitu ntakavyokwenda navyo ewura....

Msaada jamani naona kama muda unakimbia napoteza muda.....
Ewura lazima waangalie eneo ndiyo upatiwe kibali cha ujenzi wa kituo.
 
Kuna aina mbili za hivyo vituo!aina kwanza jenga cha kwako....kwa standard ya (seek ushauri kwa Oilcom,Gapco,Total etc) ambao watakuuzia hayo mafuta!unakuwa unatumia logo yao .....ukishajenga kituo,unaweka deposit kwao mnaanza biashara!unaletewa mzigo ukiuza unapeleka hela yao ww unabakia faida....wanaleta tena!ila lazima uweke deposit kama 150m hivi!ama la uwe unanunua cash bin cash...hakuna kuchagua kampuni ya kukuuzia!unaenda popote na kununua mzigo unamwaga na kuuza!wajuzi zaidi wakiamka watakumwagia zaidi!subiri
Umejibu sahihi kabisa.
 
Wakuu nimeamua kuthubutu. Nataka kuanzisha kituo cha kuuzia mafuta (petrol & diesel). Ninapanga kuanza na na pampu mbili tu. Je ni mambo yapi ya msingi ninayopaswa kuzingatia ili kuanzisha kituo?
Changamoto kubwa kwenye kituo ni evaparation of surface of liquid to gaseous,atleast 200liters per month kutokana na eneo pit tank ulipohifadhi pamoja na maeneo mfano dar na arusha zinaweza kuwa tofauti.
 
Kwa hiyo inabidi kubalance kwenye bei basi. EWURA wanalijua hili?
 
Back
Top Bottom