MIMI NILIWAHI KUULIZIA HII BIASHARA KITAMBO SANA NA NILIJIBIWA HIVI;
Mwaka 2014 niliwahi kufanyakazi GAPCO (terminal-kurasini) kipindi hiko Meneja Mkuu alikuwa mzee MOSHA kabla hajastaafu, kuna siku alikuja kukagua matenki kwenye eneo yalipojengwa matenki (farm tank).
Basi tukakutana na kwakuwa yeye alikuwa ndio boss pale akaniuliza maswali kuhusu services za matenki maana yalikuwa yanatakiwa kupigwa rangi upya, katikati ya maongezi nilimuuliza;
‘’ hivi mzee nikiwa na milioni mia sita naweza nikafungua kituo cha kuuza mafuta yaani (petrol station)? Maana haiitwi sheli.... sheli ni jina la kampuni ya kuuza mafuta zamani zileee kama leo ilivyo Total, Puma, Engen, Kobil n.k
Alinijibu hivi;
‘’kijana wangu kama umeuza nyumba ya urithi umepata hiyo pesa ni bora ufanye biashara nyingine tu, hiyo pesa ni kidunchu mno usione watu wanamiliki vituo ukadhani ni biashara ya mzaha! Hiyo pesa kama kweli unataka kufanya biashara ya mafuta labda ukodi kituo cha kampuni yoyote mfano hapa Gapco tukukodishe yaani kila kitu ni mali yetu isipokuwa wafanyakazi na mafuta utakayoweka tu ndio mali yako... tena tunakuuzia kwa masharti halafu kukipata tu hiko kituo lazima ukutane na changamoto’’
Baada ya kuniambia hivyo nikataka kujua kidogo hayo masharti na hizo changamoto zake zipoje?
Akaendelea kusema;
‘’ 1.kwanza mafuta lazima unnue kwenye terminal ambayo inamiliki kituo mfano kama kituo chako ni Gapco huruhusiwi kunnua terminal nyingine hata kama bei imepanda au kukiwa na upungufu wa mafuta inakubidi usubiri sio kunnua kwingne.
2.Mafuta unapangiwa ujazo (lita) za kununua kwa kila mwezi na hiyo ipo kwenye mkataba, mfano unaweza kuambiwa kwa kila mwezi unatakiwa kunnua lita 80,000 ni lazima unnue haijalishi kama hauuzi hiyo ni juu yako lazima unnue kila mwezi.
3.Pamoja na kuwa unanunua mafuta yao lakini kituo unakilipia kodi kama kawaida.
4.Na ili upate wateja wengi lazima uwe na msingi mkubwa yaani biashara ya mafuta mwenye msingi mkubwa ndio mwenye wateja wengi.....kivipi?
Ipo hivi unapouza mafuta kuna watu watanunua kwa cash (hawa huwa hawanunui mafuta mengi) na kuna kampuni ambazo (hazitanunua kwa cash yaani wao wanapohitaji unawajazia unaandika mwisho wa mwezi mnapiga hesabu unalipwa) kampuni hizi utakuta zinamiliki magari madogo, malori au mabasi yanayokwenda mikoani mfano unapata kampuni moja tu ya NEW FORCE hebu fikiria lile basi moja kutoka dar mpaka sumbawanga linatumia lita ngapi? (takribani mia tatu). Halafu jiulize hizo basi zipo ngapi? Zote zije kunyonya mafuta kwako kilasiku halafu malipo ni mwisho wa mwezi utaweza kumudu? (Kumbuka kila mwezi unatakiwa ufikie kiwango cha manunuzi uliyowekewa) ina maana lazima uwe na pesa ya ziada ndio maana nikakwambia kwa hiyo hela yako haitoshi.
5.kupata kituo katika kampuni yoyote ile ni kama kupata nyumba ya NHC utakuta mtu mkataba wake unaisha baada ya miaka mitano ijayo lakini kuna watu wengine si chini ya wanne au watano na wao pia washatoa order ya kukitaka endapo atashindwa biashara au mkataba wake ukiisha...kwa ufupi ili uweze kupata uwe mpambanaji haswaa!
KUMBUKA HII ILIKUWA MWAKA 2014
NA SASAHV GAPCO IMEUZWA INAITWA TOTAL