Uhuru24
JF-Expert Member
- May 2, 2015
- 4,112
- 4,361
Hahahahhahahhaha
Ndio maana ukaambiwa hiyo pesa ni ndogo sana,
Duniani hakuna mfanyabiashara anayependa kukopesha hakunaa! Isipokuwa watu wanakopesha ili biashara iwe na mzunguko mzuri bidhaa iliyopo itoke nyngine inunuliwe.
Huwezi kumudu biashara ya mafuta kama si mkopeshaji, hata mabenki na taasisi hukopesha lengo ni kupata wateja (wanachama) sambamba na ushindani wa kibiashara, mtu hawezi kuja kunnua kwako kilasiku anatoa cash wakati jirani yako kampa ofa ya kukopa kilasiku.
Kwanini inakulazimu ukopeshe?
Ukisoma vizuri kwenye komenti yangu ya mwanzo nimeandika kuwa kwenye mkataba moja ya makubaliano unapangiwa kiwango cha manunuzi mfano; Petrol kwa mwezi utannua lita laki tatu inamaana uwe na uwezo na uhakika wa kuuza lita elfu kumi kilasiku hiyo ni petrol.. Diesel kwa mwezi utannua lita laki sita hapa inabidi kilasiku lazima uuze diesel si chini ya lita elfu ishirini..
Ukisema unataka cash ndugu mafuta yatabaki mengi kwenye tenki (kisima) chako, na unatakiwa ukachukue mengine depot (terminal) utayaweka wapi haya mengine?