Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Osha mchele ulioondolewa taka. Weka kwenye sufuria na maji yawe mara tatu kwenye kufunika maji. Weka chumvi kidogo na siagi. Pika huku ukikoroga mara kwa mara hadi uwive.
kwa ladha zaidi unaweza kuuchemsha mchele kwa maji yaliyochanganywa na maziwa ama nazi.
mmmmh hapa unamwelekeza mpishi aliyesahau ... au ambae hajui kabisaaa ... maaana ..
Heh, unataka aelekezwe kama kwenye tv? Washa jiko, chukua sufuriaa safi weka motoni?
i presume ni mpishi tayari.
Ila kwa kweli kama mtoa mada bado sijaelewa vema namna ya kuupika, naomba kueleweshwa zaidi tafadhali
huwezi sema unamfundiaha mtu kitu alafu unasema unapresume ...
kama unajua toa Elimu iliyoeleweka
Anza somo tu upya mkuu wangu ili kesho asubuhi niupike kwa utulivu
Wewe ni mwanafunzi mvivu! Nimekupa maelekezo, kama kuna part hujaelewa uliza. Tatizo mie sio mwalimu wa UPE, kufundisha a e i o u sijui! Rudia kusoma post, kama una swali uliza. Hujaelewa nini???
ww hujaelewa banah kabisaa yani .. rudia tu .. sio lazima kila kitu ' jf '
Duh,
Mmenikumbusha mbaaaali sana.
Huu uji nilikuwa naumind saaana tu.
Kuna huu, halafu kuna mihogo ya nazi, halafu kuna njegere za nazi.
My mouth is watering as I am typing this.
Nakumbuka wimbo wa Abeti Masikini alivyokuwa anakumbuka vyakula vya kwao.
"Nalupilipili mwaa, na lu chumvi mwa linakolea kwa kichwa
Manjano na mdalasini eeh, manjano na mdalasini, popopo, waa"
My mom huchukua wali uliobaki mchana anauongezea maziwa na sukar na hiliki ..tunakula usiku. Tumemaliza.
uhindini unaitwa kheer.
Cc. farkhina & Punjab Singh
Kwa vile hamuwezi kuuliza masuali ya ufahamu, ngoja niwaulize mie.
kwa nini unataka kupika uji wa mchele?
unajua kuna uji wa mtama na ulezi pia? Na zote zina faida zake mwilini?