Msaada wa namna ya kupika uji wa mchele

Msaada wa namna ya kupika uji wa mchele

oxlade

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2012
Posts
601
Reaction score
96
niupikaje huo uji jamani, msaada wa hatua na vinavyohitajika. asante
 
Chemsha mchele kisha saga ,halafu tia tui sukari chumvi kidogo na hiriki.
 
Osha mchele ulioondolewa taka. Weka kwenye sufuria na maji ya moto yawe mara tatu kwenye kufunika mchele. Weka chumvi kidogo na siagi. Pika huku ukikoroga mara kwa mara hadi uwive.

kwa ladha zaidi unaweza kuuchemsha mchele kwa maji yaliyochanganywa na maziwa ama nazi.
 
Duh,

Mmenikumbusha mbaaaali sana.

Huu uji nilikuwa naumind saaana tu.

Kuna huu, halafu kuna mihogo ya nazi, halafu kuna njegere za nazi.

My mouth is watering as I am typing this.

Nakumbuka wimbo wa Abeti Masikini alivyokuwa anakumbuka vyakula vya kwao.

"Nalupilipili mwaa, na lu chumvi mwa linakolea kwa kichwa
Manjano na mdalasini eeh, manjano na mdalasini, popopo, waa"
 
Osha mchele ulioondolewa taka. Weka kwenye sufuria na maji yawe mara tatu kwenye kufunika maji. Weka chumvi kidogo na siagi. Pika huku ukikoroga mara kwa mara hadi uwive.

kwa ladha zaidi unaweza kuuchemsha mchele kwa maji yaliyochanganywa na maziwa ama nazi.

mmmmh hapa unamwelekeza mpishi aliyesahau ... au ambae hajui kabisaaa ... maaana ..
 
Heh, unataka aelekezwe kama kwenye tv? Washa jiko, chukua sufuriaa safi weka motoni?

i presume ni mpishi tayari.
mmmmh hapa unamwelekeza mpishi aliyesahau ... au ambae hajui kabisaaa ... maaana ..
 
Heh, unataka aelekezwe kama kwenye tv? Washa jiko, chukua sufuriaa safi weka motoni?

i presume ni mpishi tayari.

Ila kwa kweli kama mtoa mada bado sijaelewa vema namna ya kuupika, naomba kueleweshwa zaidi tafadhali
 
Heh, unataka aelekezwe kama kwenye tv? Washa jiko, chukua sufuriaa safi weka motoni?

i presume ni mpishi tayari.

huwezi sema unamfundiaha mtu kitu alafu unasema unapresume ...

kama unajua toa Elimu iliyoeleweka
 
Ndo nshamaliza hapo kaka. Tiririka unirekebishe nilipopunja. Mfano ungependelwa niongezee nini hapo?
huwezi sema unamfundiaha mtu kitu alafu unasema unapresume ...

kama unajua toa Elimu iliyoeleweka
 
Wewe ni mwanafunzi mvivu! Nimekupa maelekezo, kama kuna part hujaelewa uliza. Tatizo mie sio mwalimu wa UPE, kufundisha a e i o u sijui! Rudia kusoma post, kama una swali uliza. Hujaelewa nini???
Anza somo tu upya mkuu wangu ili kesho asubuhi niupike kwa utulivu
 
Wewe ni mwanafunzi mvivu! Nimekupa maelekezo, kama kuna part hujaelewa uliza. Tatizo mie sio mwalimu wa UPE, kufundisha a e i o u sijui! Rudia kusoma post, kama una swali uliza. Hujaelewa nini???

ww hujaelewa banah kabisaa yani .. rudia tu .. sio lazima kila kitu ' jf '
 
Kwa vile hamuwezi kuuliza masuali ya ufahamu, ngoja niwaulize mie.

kwa nini unataka kupika uji wa mchele?

unajua kuna uji wa mtama na ulezi pia? Na zote zina faida zake mwilini?
ww hujaelewa banah kabisaa yani .. rudia tu .. sio lazima kila kitu ' jf '
 
My mom huchukua wali uliobaki mchana anauongezea maziwa na sukar na hiliki ..tunakula usiku. Tumemaliza.
uhindini unaitwa kheer.

Cc. farkhina & Punjab Singh
 
Last edited by a moderator:
Duh,

Mmenikumbusha mbaaaali sana.

Huu uji nilikuwa naumind saaana tu.

Kuna huu, halafu kuna mihogo ya nazi, halafu kuna njegere za nazi.

My mouth is watering as I am typing this.

Nakumbuka wimbo wa Abeti Masikini alivyokuwa anakumbuka vyakula vya kwao.

"Nalupilipili mwaa, na lu chumvi mwa linakolea kwa kichwa
Manjano na mdalasini eeh, manjano na mdalasini, popopo, waa"

Lol, mi mara ya mwanzo kunywa uji wa mchele nilishangaa kuona una chumvi, nkaomba sukari kuweka sukari ukawa haunyweki. Watu wote walicheka. Ama kutoka siku hio hadi leo sijautia kinywani
 
Kwa vile hamuwezi kuuliza masuali ya ufahamu, ngoja niwaulize mie.

kwa nini unataka kupika uji wa mchele?

unajua kuna uji wa mtama na ulezi pia? Na zote zina faida zake mwilini?

Huu ni ukorofi mwelekeze basi mwenzio khaaa
 
Mambo ya mapishi yana wenyewe.

Mie kanuni yangu moja tu, kitu kiive basi. Najua hata ukichanganya mbilimbi na viazi ukavichemsha ipasavyo vitalika tu.

Sasa huo uji mbona rahisi tu, si unamwagia ubwabwa kwenye uji uliochemka ama? Ukipenda unayunyuzia pilipili manga kwa mbaaaaaali kisha vumba la mdalasini. Yanini kujizonga?
 
Back
Top Bottom