Msaada wa namna ya kupokea fedha kutoka nje ya nchi

sir kiduku

Member
Joined
Oct 12, 2019
Posts
86
Reaction score
213
Habari za muda huu ndugu zangu.

Napenda kufahamu kama kuna mtu mwenye uzoefu la hili swala anielekeze. Kwa anayefahamu application ya skrill inayotumika kutuma pesa kutoka nnje ya nchi kuja hapa kwetu tanzania na pia inafanya hvyo dunia nzima.

Naomba anifahamishe zaidi namna ya kupokea pesa na jinsi ninavyoweza zihamishie kwenye account yangu ya bank.

Au kama ninaweza kupata hizo pesa kutoka nje ya nchi kuja kwenye account yangu moja kwa moja pia naomba mnisaidiee wakuu kunielewesha hapo.

NB: Nchi ni USA kuja hapa bongo
Na account ya bank ni NMB.

Shukrani naamini nitapata majibu.
 
Mwambie akutumie via xoom. Kama yuko US bila shaka ana account ya paypal na hiyo automatically inamfanya au na account ya xoom. So atumie xoom kukutumia pesa atachagua iingie kwa simu au account.
Njia nyingine atumie wise napo kama hana account atafungua acc ni simple tu dakika 2, then aunge kad yake bank achague kukutima via simu au acc ya bank
 
Huwa anatumia skrill kwenye transaction zake hana paypal
 
Skrill unatuma direct kwenye account ya bank hata ile bank ya maendeleo vijijini aka crdb unapata mpunga wako chap.
 
Mi huwa napokea Kwa M-pesa toka US mkuu,hata juzi kuna harusi ya mshikaji mi Muhasibu,hela zimetumwa fresh M-pesa labda kama ni kiasi kikubwa unataka kiingie Bank ila hizi 10m kushuka M-pesa inapokea bila mizengwe
 
Skrill unatuma direct kwenye account ya bank hata ile bank ya maendeleo vijijini aka crdb unapata mpunga wako chap.
Skrill makato makubwa sana mkuu. Wewe unatumia bank gani?
 
Mi huwa napokea Kwa M-pesa toka US mkuu,hata juzi kuna harusi ya mshikaji mi Muhasibu,hela zimetumwa fresh M-pesa labda kama ni kiasi kikubwa unataka kiingie Bank ila hizi 10m kushuka M-pesa inapokea bila mizengwe
Ko hadi usa kuna MPESA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…