Msaada wa Namna ya Kutengeneza Mtindi

Msaada wa Namna ya Kutengeneza Mtindi

Akili 09 Nguvu 01

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2015
Posts
695
Reaction score
1,377
JF Wataalamu wa Mapishi mko pouwa?

Mimi ni mdau wa maziwa, mara nyingi nimekuwa nikimwaga maziwa kwakuwa nashindwa kuyanywa kwa wakati
Nimeona ninusuru hali hiyo kwa kuyatengeneza kuwa Mtindi
Naombeni Msaada wa Namna bora ya Kutengeneza Mtindi kutoka kwenye Maziwa mabichi ya Ng'ombe.
Nataka nipate Mtindi safi kabisa kama ule wa Asas au Tanga fresh.
Ahsante
 
ni vema maziwa yakawa yalishachemshwa kabisa ili kuua bacteria. Kama unataka kutengenza mtindi unachukua maziwa yako fresh kisha unachanganya na maziwa mtindi kidogo kama kijiko cha chakula au robo gilasi kisha unayaacha yalale ukiwa umefunika, usiweke kwenye friji mpaka yagande. yanachukua siku 1-3 kuganda kutegemea na joto la mkoa uliopo, yakishaganda koroga tayari kwa kuliwa.

NOTE: Maziwa fresh huchanganywa na maziwa mtindi kidogo ili yagande, inaitwa kuzimua. kwa hivyo ili ugandishe utahitaji maziwa fresh mfano lita 5 na maziwa mtindi robo gilasi
 
Yakugandisha mwenyewe yanakuwa mabaya kama chips za kukaanga mwenyewe
 
Ukitaka yatoke kama Asas au tanga fresh fanya hivi chemsha maziwa acha yapoe yawe vuguvugu kama ya mtoto kunywa, weka kwenye chombo cha kugandishia changanya na mtindi kidogo unaweza nunua tanga fresh au Asas dukani , kisha funika chombo chako kisipitishe hewa kisha fanya hivi " mimi huwa natumia kindoo kugandishia kwa hiyo huwa naweka kindoo katikati ya blanket kisha natia kwenye box nafunika box naacha kwa saa 18 mpaka 24 ndo natoa nakoroga natia kwenye friji "
IMG_9459.jpeg
 
Kuna kitu wanatumia kufanya maziwa yawe mtindi hao wa viwandani,kwanza wanayatreat kwenye joto Kali,pili wanaweka "kimea" hiki ndo chanzo Cha mtindi mzuri..ndo mana watu wengi hapo wamekupa njia ya kienyeji ni kuchanganya na mtindi wa dukani kiaogo ndipo utafanikisha,ni sababu hayo ya dukani yaliekwa hiko kimea ndo kinafanikisha mgandisho.

Pia baada ya kimea Kuna kingine kinaitwa stabilizer
Kinabalansi maji kwenye mtindi,mtindi unakuwa vile una muonekano mzuri hata ukisimama mda mrefu maji hayajitengi Kwa juu.
Hii pia wanawekaga kwenye peanut butter mafuta yasijitenge Kwa juu..na vingine vingi.
Kama unaweza kwendaaduka ya preservatives ukawatajia hivo vitu wakakufundisha namna ya kutumia.utatengenza hata ndio nzima na yatadumu hata mwezi
 
JF Wataalamu wa Mapishi mko pouwa?

Mimi ni mdau wa maziwa, mara nyingi nimekuwa nikimwaga maziwa kwakuwa nashindwa kuyanywa kwa wakati
Nimeona ninusuru hali hiyo kwa kuyatengeneza kuwa Mtindi
Naombeni Msaada wa Namna bora ya Kutengeneza Mtindi kutoka kwenye Maziwa mabichi ya Ng'ombe.
Nataka nipate Mtindi safi kabisa kama ule wa Asas au Tanga fresh.
Ahsante

Umeeleza vizuri
Nyongeza; yale maziwa ya pacti unaweka kidogo ili kupata bacteria wa kugandisha maziwa.
Inamaana, ukisha gandisha maziwa yako, unaweza kuacha kidogo yaliyo ganda ukaweza kuyatumia kwa awamu nyingine kwa kuyachanganya na maziwa fresh badala ya kununua ya pact
 
Zamani nakumbuka bibi alikuwa anaweka kitu kama Jani la mhindi analisafisha then anaweka ktk maziwa fresh.
 
Back
Top Bottom