Nautical Miles
Member
- Jul 2, 2024
- 7
- 3
Wakuu salaam,
Awali ya yote nawashukuru wana Jamii forums wote kwa michango yenu na mawazo yenu yakinifu yanayo toa elimu, ushauri na msaada mkubwa sana kwa jamii.
Mimi ni kijana wa kiume mwenye umri wa miaka 22 mkazi wa Dar es salaam. Elimu yangu ni kidato cha sita (High school). Baada ya kuhitimu elimu ya kidato cha sita niliamua kujifunza lugha ya kijerumani nikiwa na malengo ya kwenda ughaibuni hasa nchini Ujerumani kutafuta fursa za kazi pia kujiendeleza kimasomo.
Baada ya kujifunza lugha ya kijerumani na kufanya research ya kina ya aina gani ya viza naweza kuomba kulingana na elimu yangu na umri wangu, Nime plan na nina mpango wa kuomba viza ya
"AU-PAIR" nchini Ujerumani.
AU-PAIR ni viza ambayo inamwezesha kijana yeyote mwenye umri kati ya miaka 18-26 kwenda nchini Ujerumani kwa mwaka mmoja kufanya kazi na familia(Host family), Kulea watoto na kufanya shughuli zingine na familia husika huku akijifunza lugha ya kijerumani zaidi na kupatiwa malipo ya kujikimu.
Kisha baada ya mwaka mmoja kuisha unaweza ku extend viza yako kwaku apply university au voluntary social works zingine na kuendelea kusalia Ujerumani.
Nakuja mbele yenu wakuu, Kuomba msaada wa sehemu ya kujitolea kwenye Nursery school au Daycare ili niweze kupata "Referees na Recommendation letter" itakayo nisaidia ubalozini kuthibitisha kwamba nimefanya kazi ya kujitolea na nina uzoefu wa kulea na kukaa na watoto nchini kwangu.
Kwa sasa napatikana
Dar es salaam- Kimara. Nipo tayari kufanya kazi yoyote ya kujitolea angalau kwa miezi 2 kwenye Nursery schools au Daycare yeyote hapa Dar es salaam.
Nahitaji msaada wenu wakuu, Kwa yeyote mwenye Nursery school au Daycare au ana connection na wahusika wanaoweza kunisaidia nikajitolea kisha wakaniandikia recommendation letter, Anisaidie🤲
Mtaani bongo pamoto sana wakuu.😔
Kwa yeyote mwenye experience na aina hii ya viza ya
AU-PAIR naomba maoni yako na ushauri.
PM yangu iko wazi wakuu
Nawasilisha kwenu, Naombeni msaada wenu.