Mchokozi wa mambo
JF-Expert Member
- Mar 27, 2014
- 201
- 159
Naomba msaada jamani wana JF kuhusu hili:-
Mimi nimehitimu elimu ya Sekondari mwaka 2008 lkn bahati mbaya matokeo yangu hayakuwa mazuri sana ya kuniwezesha kuendelea na kidato cha V, lakini wakati nafikiria na kutafakari jinsi gani nitafanyeje ili niweze kujiendeleza au kurudia mtihani 2009 baba yangu mzazi alifariki.
Lakini sikukata tamaa ya kusoma mwaka 2010 niliweza kurudia mtihani wa kidato cha nne kufanikiwa kupata credit 4 za Physics, Chemistry, Geography na Kiswahili na Masomo mengine yaliyobaki nilipata alama D. Lakini wakati nafanya mtihani baba yangu mdogo aliniahidi kuwa angenifanyia mpango wa kulipiwa ada ya shule katka kampuni moja ya Mgodi iliyopo mkoani Mara, hivyo nikawa nasoma kwa bidii ili nifaulu na kweli matokeo yalipotoka niliweza kufaulu.
Baada ya matokeo kutoka nikampigia simu baba yangu mdogo kumueleza kuwa nimepata credit za kuniwezesha kuendelea na kidato cha V. Lakini baba mdogo alinijibu kuwa ule mpango umesitishwa mwenye kampuni amegungua kuwa pesa alikuwa anatoa serikali za mitaa kwa kushirikiana na halmashauri wanatafuna bila kufika kwa walengwa.
Kwa kweli jamani nililia sana kwa kukosa tena ufadhili wa kusomeshwa na hali uwezo wa kimasomo ninao. Hata hivyo mwaka 2011 nilikutana na dada ambaye wakati ninaanza form I yeye alikuwa form IV akaniuliza wewe uko wapi siku hizi, nikamuelezea kitu, alisikitika sana alichoniambia ni kwamba nielendelee kutafuta angalau kiasi fulani wakati yeye alikuwa anakaribia kumaliza chuo Muhimbili akipata kazi ataniwezesha niweze kwenda College.
Na kweli niliweza kuanza mradi wa kufuga kuku wa nyama 50 kwa kutumia sehemu ambayo nilimwomba shangazi yangu... mwaka huu nilikuwa nimefikisha mradi wa kufuga kuku 250 na kuna sehemu ambayo nilikuwa nanunua chakula cha kuku na mwezi hiyo sehemu nikakuta wameanza kuleta vifaranga wa kuku wa nyama na mimi nikavutiwa kuchua hapo hapo vifaranga na chakula ili kuepuka gharama maana ilikuwa ni sehemu ya karibu na nyumbani.
Mwezi June, nilienda kuoda vifaranga 250 hiyo sehemu, wakaniambia njoo siku fulani uchukue vifaranga, siku ilipofika akaenda kunichukulia shangazi yangu maana mimi siku hiyo nilikuwa Kibaruani. kweli kwa macho vifaranga walikuwa wanaonekana wana afya nzuri, lakini baada ya siku2 tu wale vifaranga walianza kupooza miguu na kushindwa kutembea na wengine kuanza kufa.
Siku ya 3 nikatoa taarifa kwa yule aliyeniuzia vifaranga alichoniambia ni kwamba kuna madaktali wa ile kampuni ya vifaranga watakuja kuwachech lakini wakakaa wiki nzima sikuwaona. Nikaamua kwenda tena yule agent wao akanichukua kwenda watu ambao tulichukua vifaranga siku moja nione wakoje maana vifaranga wao ni wazima kabisa, nikaenda na kuwaona lakini nilichokigundua ni kwamba wale vifaranga ni tofauti kabisa na wale wa kwangu..
Kumbe vifaranga niliopewa ni tofauti na watu wengine. Niliporudi nyumbani nilimtumia msg yule agent wao kumueleza kuwa vifaranga ambao ulinipa sio sawa na wale uliowapa watu wengine kwanini?
Agent yule akaforward ile msg kwa meneja masoko wa ile kampuni ya vifaranga wakatuma watu wawili waje kuona ni tatizo, walipofika kweli waliowaona wale vifaranga na wengine walikuwa wamekufa wakawapiga picha na kutembelea vifaranga wa majirani wengine, wakasema wanapeleka taarifa kwa bosi wao.
Chakushangaza hawa jamaa waliishia njiani zile taarifa hazikufika kwa bosi wao. nikaamua kuomba namba ya meneja masoko wa ile kampuni nikamuuliza vipi wale jamaa uliowatuma wamekupa taarifa gani? akanijibu kuwa hajapata taarifa yoyote.... akaniambia kuwa watakuja na bosi wake wa kampuni kuwaona vifaranga wangu, wakati huo wanaendelea kufa tu...
kweli siku ilipofika wakaja wakaingia bandani wakajionea hali halisi iliyopo... bosi wao alichosema ni kwamba naomba mlete box ambalo mlichikulia vifaranga, tukamletea akaliangalia na kusema hili box si la kampuni yetu isipokuwa huu mfuniko wa juu ni wa kampuni yetu maana kuna alama ambayo tunaiweke katika box la chini ambayo tunaitambua sisi wenyewe. ... Wakaondoka na kusema wanaenda kwa agent wao watanipa taarifa.
Jamani hivi ninavyoandika maelezo haya ingawa yanachosha kusoma ni kwamba hawa watu wote kwa kushirikiana na agent wao wanarushiana mpira.. Na agent wao naongea nae anakuwa mkali kama pilipili na tayari nimeisha ingia hasara ya kuwarisha wale vifaranga na muda wa kuuza umefika nimeuza vifanga 80 tu na tayari wamekufa vifaranga 63 mpaka sasa, lakini waliobaki wote hawatembei.
Wana JF naomba kwa mtu ambaye anaweza kunisaidia kudai haki yangu ya fidia juu ya hasara ambayo wamenisababishia na mimi sasa msingi wa kufuga tena umekatika nina mawazo sana kwa kweli kuna muda ukifika nashindwa hata kula ukizingatia vipindi vigumu vyote nilivyopitia na kuna msamaria mwema alikuwa ameniahidi kuwa atanisaidia kulipa ada ya chuo lakini lazima na mimi niwe na kiasi kadhaa.... tayari nilikuwa nimeapply nafasi 3 za kusoma vya serikali ninasubiri post nikasome.
Sijui la kufanya jamani nisaidini hata kwa ushauri tu.. na Mungu atawalipa kwa sehemu mliojitolea kunisaidia maana lengo langu ni kusoma na familia yetu ya watoto 11 ni masikini sana na hakuna hata ndugu yangu mmoja aliyefika angalau Sekondari, mimi ndiye wa kwanza kufika ngazi hii ambayo ni ya chini sana, natamani nisiishie hapa bali nielendelee mbele bila kukata tamaa. Hawa watu walionisababishia hasara hii kwa sababu wana pesa, wananidharau sana kwa sababu sina pesa.
:cool2:
Asante,
kwa ushauri zaidi unaweza pia kunitumia email kupitia:- abc.nect@yahoo.com au namba ya Simu:0753 852631