Ndugu negligible kwanza inaonekana hujapatwa na hili tatizo ila unataka kujua kama ikitokea uchukue hatua gani zinazositahili.Ikiwa hivyo ndivyo basi utakuwa na mda zaidi wa kuendelea kutafiti juu ya suala lako au umesha tafiti tayari.
Kwa uelewa wangu mdogo najua suala hili litaangukia chini ya sheria za madhara(law of Negligence) katika sheria hizi huwa haitegemei upande wa pili kama mlikuwa na mkataba naye au la.Vitu ambavyo utatakiwa kuthibitisha ni je,huyo mtu alikuwa na wajibu ambao alitakiwa autekeleze,na je huo wajibu hakuutekeleza na matokeo ya kuto tekeleza ndio yamekusababishia madhara wewe.Kama utakuwa unauwezo wa kuthibitisha hayo unaweza kupeleka madai yako.
Lakini haya ni mambo ya kimahakama zaidi ambayo si vizuri kukimbilia haraka pale tatizo linapotokea unaweza kuwasiliana kwanza na mhusika si ajabu yeye mwenyewe akawa ameshatambua uzembe wake na akawa tayari kukulipa uhalibifu uliotokea na au mkajadiliana kwa namna fulani ya kuchangia gharama.