Msaada wa sheria kuhusu bima

Msaada wa sheria kuhusu bima

callixtus

Member
Joined
May 7, 2015
Posts
86
Reaction score
31
Kiukweli mimi nimesononeshwa sana na hili
shirika kwanza kabisa nashindwa kuelewa
wanatuchukuliaje sisi watumishi wa chini
kabisa.Kuna kipindi huwa nafikia hatua ya
kuwachukulia kama wezi wa kisasa mfano mzur
kwa watumishi
Kuna huduma ya BIMA YA MAISHA (Bima ya
matumaini) watumishi wengi wananyanyasika na
hili niliweke wazi ni kutokana na maisha yao kuwa
magumu imefikia hatua ndo imekuwa kilio kwao
wanawashawishi watu wajiunge kwenye huduma
hizo kwa lengo la kujiwekea fedha kidogo kidogo
kwa muda wa miaka 3 halafu unapewa asilimia 20
ya pesa yako itakayokatwa kwa miaka 9 lakini cha
ajabu miaka mitatu inaweza kufika ukazunguushwa
mpaka miezi isiyojulikana na wakat huo mtu
anategemea kuipata hiyo pesa kwa ajili ya
mipango aliyojiwekea mfano mimi na kaka yangu
mtumishi mkoani simiyu hukoo vijijini alipaswa
kulipwa fedha yake tangu june lakini mpaka sasa
hajalipwa pesa na ameshasafir kwenda kwenye
ofisi zao zaid ya mara tatu na istoshe gharama ya
nauli ni sh 23000 kwenda tuuu ukizidisha kiasi
alichotumia kufuatilia pesa yake ni nusu ya pesa
anayopaswa kulipwa na hajalipwa mpaka sasa na
alishamtumia mkurugenzi wa shirika e-mail lakini
haikujibiwa Mi niwaombe NIC mjaribu kutuhurumia
wenzeni tunaotumia viatu vyenye soli zilizokaa
upande msitunyanyase kwa kuwa uwezo wa
kusimama na ninyi mahakamani hatuna tusaidieni
mtupe stahiki zetu kwenye mshahara mnatukata
kutulipa hakuna ni unyanyasaji na udharirishaji
kwa watu wenye kipato kidogo
 
Back
Top Bottom