Msaada wa sheria, Matapeli Wameniliza

Msaada wa sheria, Matapeli Wameniliza

Chozy

Senior Member
Joined
Aug 22, 2012
Posts
172
Reaction score
47
Kuna matapeli wamenipiga ambao hutumia za Tigo.

Story yenyewe iko hivi;

Nimepokea sms kutoka simu ya dada yangu ikinielekeza kutuma pesa 250,000 kwa mtu kwani ana shida sana, na akanitumia namba ya huyo mtu na jina lake, muda mfupi baada ya ujumbe kuingia huyo mtu akanipigia kama nimepata ujumbe wa dada na kudai kuwa nimsaidie haraka, nikampigia dada kuconfirm hakupokea huku nikisumbuliwa na huyu MTU, nikaona isiwe tabu wacha nimsaidie, nikatuma Tigo pesa.

Na ujumbe wa kuonyesha pesa imekwenda nikafoadi kwa dada. Dada alinipigia baada ya muda kuliza ule ujumbe nikamjulisha kilikuwa ni kitu kigeni kwake. Nikascreenshot nikamtumia kashangaa sana. Kwenda tigo ile namba haipatikani hata baada ya kupata ile pesa hakuna simu ya shukrani. Pesa katoa na simu haipatikani.

Baada ya muda nikapokea ujumbe mwingine kutoka kwa dadangu huyohuyo ukinitaka nimsaidie mtu mwingine 400,000 jina na nambayake, huyu wa sasa akapiga simu namba tofauti na ile ya kwanza hata sauti pia akijieleza kwa jinsi walivo karibu na Dada hivyo Dada kaniomba nimsaidie.

Kwa kuwa mchezo nilishaujua nilimuomba tuonane nimpe cash alinisihi sana nimtumie coz kabanwa hawezi toka nikaona isiwe tabu nimfate aliponielekeza nimpe mpunga. Kufika maeneo Yale simu imezimwa.

Nimelizwa jamani nitapaje jasho langu..
 
Hizo ni sms nilizopokea toka kwa dada kumbe ni matapeli wamehack nambayake
 
Attachments

  • 1424793312475.jpg
    1424793312475.jpg
    16.5 KB · Views: 1,436
  • 1424793362012.jpg
    1424793362012.jpg
    31.7 KB · Views: 1,219
daaah pole mkuu nimebakiwa na maswali mengi ambayo siwezi yapatia majibu
 
Pole sana jaribu kuongea na tigo wanaweza wakakupa msaada
 
Kwani hiyo number haijasajiliwa?Hawawezi kuangalia kuona nani anae wasiliana nae sana ili kumkamata?

Wameangalia imesajiliwa 2013 lkn imeanza kutumika tarehe 21 Feb 2015 na namba iliyowasiana zipo 6 na yangu ikiwemo nimepewa hizo namba 2 za airtel ndo ziliwasiliana marakwamara baada ya kunipigia mimi
 
Ni wizi wa akiri ambao umeanza kwa kuconnect namba ya mtu ambaye ni mtu wa karibu na wanacheza na maswala ya mtandao hii imetokea kwa jirani yangu adi kesi kaipeleka polisi ila mimi nimemwambia ameishatapeliwa.
 
Unafikiri service provider wanahusika na hawa matapeli?
 
Kwani hiyo number haijasajiliwa?Hawawezi kuangalia kuona nani anae wasiliana nae sana ili kumkamata?

Hizi namba zinazosajiliwa vijiweni kwani zina udhibiti? Unasajili hata kama huna kitambulisho, tena kuna vidada mpaka vinatembeza mpaka majumbani vikikaa vibaya unavifagia kwenye yale mambo yetu!! Ndugu yetu awe mpole tu hicho hakirudi tena!!
 
Duh! Asalalleh!!
 
Hizi ndio negative effects za kukua kwa teknolojia.
Mkuu hizo ni bulk SMS ambazo unaweka sender ID yoyote uitakayo. Ni fake SMS usipokuwa makini MTU yoyote anaweza kuibiwa. Na haswa namba za tigo na airtel zina accept hizo spam meseji. Hawa jamaa wamezagaa sana hapa mjini wanawaliza watu wengi nishashuhudia MTU kaibiwa 5M.

Staili nyingine ni hii, ananunua kitu kwako cha hela nyingi alafu anakwambia sina cash nakulipa kwa m-pesa. Kisha atakuomba namba ambayo sio ya M-PESA atakupa maneno matam ili uingie tego lake. Atakwambia hivi nikutumie toka mtandao mwingine ili hela ya kutolea nikatwe Mimi na wewe ifike kwako hela kamili. Kwa kuhofia withdraw charge lazima utaingia kwenye tego. Hawezi kukubali kutuma kwenye same network kwasababu mwisho wa Meseji utakayopokea itaonesha Salio ambalo ukiona liko tofauti lazima utashtuka.
Ushauri. Cash ndio mpango mzima usikubali akulipe kama nilivyoainisha hapo juu.

Hizo issue inatakiwa uwaone polisi kitengo cyber crime watakusaidia. Japo watakuzungusha. Lazima watatrack source ya ile Meseji na wale walio pokea hela.
Pole sana mkuu!
 
Asante sana, ndo tunajifunza Siku nyingine tuwe makini na hizi e - trx
 
Duh watu waweza kuibiwa kirahisi hivyo? pole sana
 
Huo wizi upo tangu mwishoni mwa mwaka Jana mi wamejaribu wakashindwa make mi ndo nahudumia na ndo mwenye duka sasa wakituma kwa msichana wangu na Mimi nakuwepo hapohapo kwahiyo tunawaenjoy but mwanzoni ilinipa shida kutambua simu yangu wameipata wapi kutuma SMS kwa msichana wangu.
 
pole ila ukipeleka polis jamaa wa cybercrime hatusaidiwa na utakua umewapelekea deal deal tu hadi RCO ilala ndio balaa
 
Back
Top Bottom