Kuna rafiki yangu amefanya kazi kenye shirika miaka 28,mwajiri akaamua kumfukuza kazi,kitendo ambacho jamaa yangu hakuridhika nacho. Akaenda CMA ambao wametoa hukumu yao kwamba arudishwe kazini.Mwajiri akaamua kumuandikia kuwa asubiri atafute taratibu nyingine.Sasa imepita zaidi ya mwezi sasa jamaa haelewi afanyeje?Anaomba kujua taratibu gani sasa afuate ili apate haki yake.