Msaada wa sheria ya kazi

Msaada wa sheria ya kazi

Hollyreath

Senior Member
Joined
Apr 22, 2013
Posts
126
Reaction score
12
Mama yangu amefanya kazi kama mwalimu wa awali kwa miaka 19 akiishi eneo la shule ilipo.Amepaendeleza na kupaboresha.

Hakuwahi kupewa likizo wala pesa zake hazikuwahi kupelekwa mfuko wa jamii.Sasa ameachishwa na amelipwa milion 1.4 kama pesa ya kiinua mgogo.

Jaman msaada aende wapi asaidiwe?

Yupo anaishi Mwanza sasa.
 
aende kwenye Ofisi za Idara ya Kazi zilizoko hapo Mwanza(mjini) Maafisa wa Kazi watampatia utaratibu wa jinsi ya kufanya lakini mwisho wa siku itabidi ajaze fomu maalumu ijulikanayo kama CMA F.1 na kuiwasilisha kwenye Ofisi za Tume ya Usuluhishi na Uamuzi-CMA zilizoko kwenye jengo hilohilo la Idara ya Kazi...baada ya hapo kinachofuta ni pande zote mbili kuudhuria kwa ajili ya kusikiliza shauri kwa hatua ya awali
 
Back
Top Bottom