Sijui off road unamaanisha nini hasa, ila 3 series haifai kwenye hilo. Iko chini saana na suspension ni sporty. Kwenye Forester na X3, binafsi nitakwenda Forester, model ya kuanzia mwaka 2008. X3 ya kwanza haikuwa nzuri kuvile, ni kama jamaa walikuwa wanajifunzia hapo kuingia kwenye segment ya small SUVs. Ila Forester 2nd and 3rd gen ziko poa.
Ulaji wa mafuta, X3 iko vizuri, kama utachukua ya engine ndogo. Forester iko juu kidogo kwenye mafuta sababu ya AWD.
Kwenye off roading, the Forester is a clear winner hapo.