Msaada wa taarifa kuhusu kilimo cha mpunga - Ifakara, Morogoro

We jamaa umemshauri vizur sanaaa huyu mtoa mada,nishauri azingatie ushaur ila anategemea anataka kulima ili apate nini?ataka kilimo biashara au?si kila anae Lima anataka kuuza ila km anataka kuuza basi husilime Mzee,hata Mimi Na mwenzangu tulitaka kulima ila baadae baada a kukaa miezi mitatu kwa maana nwanzo wa msimu mpk hiv sasa wanapo anza kulima tunaona hakuna haja ya kulima tena,tunaona ni Bora tununue mpunga Na kuweka storage somewhere! Hakika gharama za kulima ni kubwa sanaaaa! Na ni pata potea!

Sisi tumeamua kwanza tununue mpunga msimu wa mavuno.

Pili kwa kuwa tuna taasisi yetu tunakopesha basi tunakopesha wakulima Na msimu w mavuno wanalipa mpunga badala ya pesa!

Tatu,tunawataftia soko zuri wakulima ambao tumewakopeaha pesa zetu kwa mpunga wa ziada unao bakia baada ya kulipa deni letu!
 

Mnafanyia wapi shughuli zenu? Wafanyabiashara wengi waliofaidika na biashara ya kilimo hawajalima kama Export trading company, MO Dewji sidhani ni kitu kimoja na Export trading company. Ila kulima ni kuzuri inategemea na aina ya zao. Mazao yanayohitaji maji mengi kama mpunga ukitaka kulima kwa uhakika lazima uwe na uhakika wa maji (kumwagilia) nje ya hapo waweza kulia. Kilimo chochote hasa large scale ukitaka kufanikiwa lazima uwe na uhakika wa maji kabla hujafanyakitu kingine chochote kile otherwise utapoteza pesa. Nimelima hekari zaidi ya ishirini za mananasi naona jua limeniumiza sana ingawa yamezaa, yangezaa zaidi na kuwa makubwa zaidi kama ningekuwa na maji. Maji ni kila kitu kwenye kilimo.
 
Hata mimi baada ya kufanya research zangu tayari nilishabadili mawazo, nasubiri msimu wa mavuno niwe na nunua mazao badala ya kulima hasa baada ya kugundua mashamba mengi yako mbali na muda wa usimamizi utakuwa mtihani!

Nashukuru sana kwa nyote mliotoa ushauri hasa hasa hao waliozungumzia kilimo cha miwa!
 
Kama unaweza kufika CHITA nako kuna mashamba mazuri sana yana milikiwa na JKT huwa wanakodisha, mwaka Jana nilikodi kwa 40,000 per acr
Chita ipo umbari gani toka Ifakara..... And kuna barabara ya uhakika?
 
Kuna mtu aliniambia Geita Kuna udongo mzuri wa kwa ajili ya kilimo Cha mpunga , je Ni kweli wenyeji was huko?

Pia gharama km unatak kuanza kulima mpunga inabidi uwe na shilingapi , wakuu?
Asant.
 
Mkuu salama? Mrejesho wa kilimo cha mpunga ukoje?

Nafikiria pia kuingio huko, ni vizuri kama nitapaga ufahamu toka kwa wahusika.

Natanguliza shukurani.
 
Good
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…