Msaada wa taarifa kuhusu kilimo cha mpunga - Ifakara, Morogoro

Mimi nina mashamba ya urithi huko Mang'ula sijawahi kulima hata siku moja ila huwa yanakodishwa na watu niliowaachia, bei kwa sasa sifahamu kwakuwa hata hiyo pesa sijawahi kuiona jamaa wanakula tu. Sasas kama uko serious mimi ni wasimamishe wale wa kule ili nikukodishe wewe. Mimi nimekulia huko, kilimo cha mpunga ni kigumu sana hasa kama unafanya kwa jembe la mkono. Kuna kutayarisha shamba kwakuwa mashamba haya ni ya zamani unaanza na kulima kisha unapiga halo then unamwaga au kupanda mpunga, baadae kung'olea au kupiga dawa majani, kisha kama kutakuwa na ndege yakubidi ulinde ndege wasile mpunga. Baada ya hatua zaote hizo unafuatiwa na kuvuna, kupiga, kupepeta na kuweka kwenye magunia. Kwakuwa mashamba yote ya wiliya ya Kilombero yapo mbali na vijijini hususani kwenye barabara kuu ya Dar-Ifakara inakubidi uwe na plan ya kuhifadhi mpunga wako shambani baada ya kuweka kwenye magunia then usafirishe kwenda kijijini ambok itabidi utafute storage area kabla haujasafirisha kupeleka unakohitaji. Mimi nakushauri kwakuwa wewe si mwenyeji wa maendeo hayo kilimo hiki cha kutegemea mvua chaweza kukulaza, hivyo kama unapesa ya kutosha subiri wakati wa mavuno ununue mpunga na kufanya biashara au la wakati wa kulima nenda vijijini wakopeshe wananchi pesa kisha mkubaliane kulipwa mpunga wakati wa mavuno na akikosa then utajua cha kufanya. Upo?
We jamaa umemshauri vizur sanaaa huyu mtoa mada,nishauri azingatie ushaur ila anategemea anataka kulima ili apate nini?ataka kilimo biashara au?si kila anae Lima anataka kuuza ila km anataka kuuza basi husilime Mzee,hata Mimi Na mwenzangu tulitaka kulima ila baadae baada a kukaa miezi mitatu kwa maana nwanzo wa msimu mpk hiv sasa wanapo anza kulima tunaona hakuna haja ya kulima tena,tunaona ni Bora tununue mpunga Na kuweka storage somewhere! Hakika gharama za kulima ni kubwa sanaaaa! Na ni pata potea!

Sisi tumeamua kwanza tununue mpunga msimu wa mavuno.

Pili kwa kuwa tuna taasisi yetu tunakopesha basi tunakopesha wakulima Na msimu w mavuno wanalipa mpunga badala ya pesa!

Tatu,tunawataftia soko zuri wakulima ambao tumewakopeaha pesa zetu kwa mpunga wa ziada unao bakia baada ya kulipa deni letu!
 
Mnafanyia wapi shughuli zenu? Wafanyabiashara wengi waliofaidika na biashara ya kilimo hawajalima kama Export trading company, MO Dewji sidhani ni kitu kimoja na Export trading company. Ila kulima ni kuzuri inategemea na aina ya zao. Mazao yanayohitaji maji mengi kama mpunga ukitaka kulima kwa uhakika lazima uwe na uhakika wa maji (kumwagilia) nje ya hapo waweza kulia. Kilimo chochote hasa large scale ukitaka kufanikiwa lazima uwe na uhakika wa maji kabla hujafanyakitu kingine chochote kile otherwise utapoteza pesa. Nimelima hekari zaidi ya ishirini za mananasi naona jua limeniumiza sana ingawa yamezaa, yangezaa zaidi na kuwa makubwa zaidi kama ningekuwa na maji. Maji ni kila kitu kwenye kilimo.
 
Hata mimi baada ya kufanya research zangu tayari nilishabadili mawazo, nasubiri msimu wa mavuno niwe na nunua mazao badala ya kulima hasa baada ya kugundua mashamba mengi yako mbali na muda wa usimamizi utakuwa mtihani!

Nashukuru sana kwa nyote mliotoa ushauri hasa hasa hao waliozungumzia kilimo cha miwa!
 
Kama unaweza kufika CHITA nako kuna mashamba mazuri sana yana milikiwa na JKT huwa wanakodisha, mwaka Jana nilikodi kwa 40,000 per acr
Chita ipo umbari gani toka Ifakara..... And kuna barabara ya uhakika?
 
Kuna mtu aliniambia Geita Kuna udongo mzuri wa kwa ajili ya kilimo Cha mpunga , je Ni kweli wenyeji was huko?

Pia gharama km unatak kuanza kulima mpunga inabidi uwe na shilingapi , wakuu?
Asant.
 
Natumai mu wazima wanashiriki wa jukwaa hili.

Kama heading inavyojieleza naomba kwa mwenye uzoefu na kilimo cha mpunga maeneo ya Ifakara anisaidie taarifa kuhusu yafuatayo :-

i. Upatikanaji wa mashamba ya kununua au kukodi ukoje

ii. Msimu wa maandalizi ya shamba hadi kipindi cha kupanda na Upatikanaji wa mbegu /miche ukoje

iii. Makadirio ya gharama za uandaaji wa shamba hadi kufikia kupanda miche kwa ekari moja

iv. Mpunga ukishavunwa, wakulima wa maeneo hayo ukoje katika kuuza mazao yao.

v. Kijijini /vijiji gani vinazalisha mpunga kwa wingi na upatikanaji wa mashamba hausumbui sana.

Natanguliza shukrani zangu kwenu na natumai kupata mrejesho chanya kutoka kwenu.

Naamini JF ni kijiji chenye kila aina ya watu wenye uzoefu mbalimbali katika angle tofauti tofauti!
Thanks in advance!

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu salama? Mrejesho wa kilimo cha mpunga ukoje?

Nafikiria pia kuingio huko, ni vizuri kama nitapaga ufahamu toka kwa wahusika.

Natanguliza shukurani.
 
Mnafanyia wapi shughuli zenu? Wafanyabiashara wengi waliofaidika na biashara ya kilimo hawajalima kama Export trading company, MO Dewji sidhani ni kitu kimoja na Export trading company. Ila kulima ni kuzuri inategemea na aina ya zao. Mazao yanayohitaji maji mengi kama mpunga ukitaka kulima kwa uhakika lazima uwe na uhakika wa maji (kumwagilia) nje ya hapo waweza kulia. Kilimo chochote hasa large scale ukitaka kufanikiwa lazima uwe na uhakika wa maji kabla hujafanyakitu kingine chochote kile otherwise utapoteza pesa. Nimelima hekari zaidi ya ishirini za mananasi naona jua limeniumiza sana ingawa yamezaa, yangezaa zaidi na kuwa makubwa zaidi kama ningekuwa na maji. Maji ni kila kitu kwenye kilimo.
Good
 
Back
Top Bottom